Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 10 09Article 562312

Soccer News of Saturday, 9 October 2021

Chanzo: Tanzaniaweb

Rais Samia aipongeza Twiga Stars

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu ameandika "Naipongeza timu yetu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) kwa kutwaa ubingwa wa Mashindano ya COSAFA Wanawake 2021. Ubingwa huu unatuletea heshima, unaitangaza nchi yetu na kutia chachu kwa vijana wetu kushiriki michezo. Naipongeza TFF na wote walioshiriki kuiandaa timu yetu," ameandika Rais Samia Suluhu Hassan.

Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake, Twiga Stars imeifunga timu ya Malawi goli 1-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa katika dimba la Nelson Mandela huko Afrika Kusini na hivyo kutangazwa kuwa Mabingwa.