Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 11 23Article 573784

Soccer News of Tuesday, 23 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Ramos yuko tayari kwa mapambano PSG, kuwavaa Man City

Ramos akiwa mozoezini na nyota wa PSG Ramos akiwa mozoezini na nyota wa PSG

Sergio Ramos Anajandaa kucheza mchezo wake wa kwanza na klabu ya Paris Saint-Germain baada ya kutajwa katika kikosi kitakacho menyana na Manchester City siku ya Jumatano katika mchezo wa Ligi ya Mbingwa.

Tangu alipotua Parc des Princes kwa uhamisho huru akitokea Real Madrid Ramos hajaweza kucheza mchezo hata mmoja sababu ya kusumbuliwa na majeraha.

Beki huyo kisiki wa kati alicheza mara ya mwisho ilikuwa ni katika michuano ya Ligi ya Mbingwa dhidi ya Mabingwa wanaoshikilia taji hilo Chelsea mchezo ambao Madrid walipoteza darajani.

Kocha mkuu wa PSG Mauricio Pochettino alithibitisha kwamba Ramos yupo mbioni kuanza kucheza pamoja na beki mwenzie Marquinhos ambaye alikosa mchezo dhidi ya Nantes.

Mchezo wa awali wa PSG dhidi ya Man City ulikwenda kwa 2-0 ambapo vijana wa Pochettino waliondoka na alama tatu muhimu magoli yakifungwa na Lionel Messi.