Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 09 13Article 557257

Soccer News of Monday, 13 September 2021

Chanzo: salehejembe.blogspot.com

Simba SC, kuendelea walipoishia

Kikosi cha Simba mazoezini Jijini Arusha Kikosi cha Simba mazoezini Jijini Arusha

Uongozi wa Simba umeweka wazi kuwa imani yao kwa msimu wa 2021/22 ni kuweza kufanya vizuri na wataanza kuonyesha ukubwa huo kupitia tamasha la Simba Day linalotarajiwa kufanyika Septemba 19.

Leo ni Wiki ya Simba ambayo inatarajiwa kuwa na matendo ya huruma kwa jamii pamoja na kufanya usafi kabla ya siku ya tamasha yenyewe ambayo ni Septemba 19, Uwanja wa Mkapa.

Kaimu Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga amesema kuwa wapo vizuri kwa ajili ya maandalizi na wanaamini kutakuwa na jambo zuri kwa mashabiki wa timu hiyo.

“Kuna mengi mazuri kwa ajili ya Wanasimba na kazi ipo palepale kutoa burudani pamoja na kuwapa kile ambacho wanastahili mashabiki wetu wa timu hii kubwa.

“Utaratibu na shughuli nyingine zote zinakwenda vizuri timu ikirudi kutoka kambini Arusha kuna mambo mengine yataendelea kutolewa ili waweze kujua hali itakuaje lakini kwa upade wa tiketi hizo zinaendelea kuuzwa,” amesema Kamwaga.