Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 09 10Article 556768

Soccer News of Friday, 10 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Simba, Yanga uso kwa uso Disemba 11

Mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison akijaribu kuwatoka viungo wa Yanga Mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison akijaribu kuwatoka viungo wa Yanga

Ratiba ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2021/22 imetangazwa leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu, Almas Kasongo.

Mechi ya watani wa jadi kati ya Simba na Yanga itakipigwa Desemba 11.

Simba na Yanga zitafungua Ligi kwa mechi ya ngao ya jamii, Mchezo ambao utapigwa Septemba 25 kabla ya Ligi kuanza Septemba 27.

Msimu uliopita Yanga alianza kwa sare mechi ya kwanza na kushinda mechi ya pili ambayo Simba walikuwa wenyeji kwa ushindi wa goli 1-0, goli la kiungo Zawadi Mauya.

Kwa hali ya vikosi ilivyo hivi sasa ni dhahiri mtanange huo utavuta hisia za wengi hasa ikizingatiwa kila timu imefanya usajili madhubuti kuimarisha vikosi vyao.