Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 07 19Article 547414

Soccer News of Monday, 19 July 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Simba yapewa kombe lao

Simba yapewa kombe lao Simba yapewa kombe lao

LABU ya Simba leo rasmi wamekabidhiwa kombe lao baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi yaNamungo huku wakishinda 4-0.

Kombe hilo Simba wamepata baada ya kutwaa ubingwa wakiwa na jumla ya pointi 83 wakiwa vinara kwenye Ligi Kuu Bara.

Mgeni rasmi katika mchezo huo alikuwa ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala ndiye aliyemkabidhi nahodha wq Simba kombe, John Bocco.

Baada ya kuchukua kombe hilo kila mchezaji wa klabu hiyo alionyesha kuwa na furaha huku wakipiga nalo picha.

Mashabiki nao hawakuwa nyuma kwani walionyesha  kuwa na furaha baada ya kuwa pamoja kwa shangwe na wachezai wao.