Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 10 14Article 563128

Soccer News of Thursday, 14 October 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

"Sina wasi wasi na washambuliaji wetu"- Nabi

Kocha Nabi na washambuliaji wa Yanga Kocha Nabi na washambuliaji wa Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga Nasriddine Nabi amesema licha ya washambuliaji wake kuanza msimu wakiwa chini lakini imani yake juu yao ni kubwa.

Katika mechi mbili za ligi kuu ambazo Yanga imecheza imefunga mabao mawili na yote yamefungwa na viungo na siyo washambuliaji wake tegemezi Fiston Mayele na Heritier Makambo.

Akizungumza na mtandao huu Nabi amesema hana shaka na uwezo waliokuwa nao wawili hao ispokuwa ugeni wa ligi ndio unawasumbua ingawa baada ya muda mfupi kila kitu kitakaa sawa kwao.

"Hawa ni washambuliaji waviwango kila mtu anajua hilo sababu walishathibitisha ubora wao tangu huko walikokuwa sasa kutofunga mabao kipindi hiki hakiwezi kuwa sababu ya kuwaona hawafai kinachowakuta mchezaji yeyote duniani kinaweza kumtokea hivyo mashabiki wawe watulivu," amesema Nabi.

Kocha huyo amesema kitu kingine kinachosababisha wachezaji hao kushindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo ni kukutana na wachezaji tofauti na wale ambao wamezoeana nao hivyo bado hawaja elewana vizuri.

Mayele amejiunga naYanga msimu huu akitokea AS Vita ya DR Congo na mpaka sasa ameifungia bao moja tu timu yake kwenye mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba huku Makambo bado akipambana kufungua akaunti yake ya mabao.