Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 11 24Article 573850

Soccer News of Wednesday, 24 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Skendo ya video ya ngono, yamtia Benzema kitanzini

Karim Bemzema Karim Bemzema

Mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, Karim Benzema, amekutwa na hatia ya kuhusika kwenye kudukua video ya ngono ya mchezaji mwenzake Mathiew Valbuena.

Benzema alishutumiwa kutaka kujipatia kiasi cha fedha kupitia mkanda huo na sasa imempelekea kuhukumiwa mwaka mmoja jela na kutozwa faini ya paundi elfu 63,000 za England sawa na Tshs 193,911,448.

Benzema ameendelea kukataa kuhusika na makosa hayo, na ikumbukwe kashfa hiyo ndiyo iliyompelekea Mchezaji huyo kutoitwa katika kikosi cha Timu ya Taifa kwa muda mrefu.

Tukio hilo lilitokea mwaka 2015 wakati Benzema na Valbuena wakiwa kwenye kambi ya timu ya taifa jambo lilopelekea wote kuondoshwa kwenye kikosi hiko kabla ya Karim kurejeshwa hivi karibuni.

Kwa mujibu wa hakimu aliyetoa hukumu hiyo, Benzema ndiye alikuwa mtu wa kati aliyekuwa akimlazimisha Valbuena kutoa fedha ili kuzima sakata hilo, jambo ambalo lilikuja kugundulika kuwa Benzema alikuwa akishirikiana na watu hao wanne ambao pia wamekutwa na hatia.

Benzema hakuwepo mahakamani wakati huku hiyo ikitolewa kwasababu anajitayarisha na mchezo wa leo wa UCL dhidi ya Sherrif Toraspol.