Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 10 10Article 562396

Soccer News of Sunday, 10 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Stars yalipa kisasi Benin, yaongoza kundi

Mfungaji pekee wa Goli la Stars, Simon Msuva Mfungaji pekee wa Goli la Stars, Simon Msuva

Timu ya Tanzania "Taifa Stars" imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya timu ya Taifa ya Benin, katika mchezo wa kundi J kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia Qatar 2022.

Kipigo hicho walichokitoa Stars ni kama kulipa kisasi kwa Benin baada ya kupoteza siku tatu zilizopita mbele ya Benin katika uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Da es Salaam.

Stars alihitajika kuhakikisha anapata ushindi katika mchezo huo, ili afufue angalau apige hesabu za kumaliza kinara katika kundi hilo, kabla ya kuingia hatua inayofuata.

Goli pekee la Stars katika mchezo huo limefungwa na Nyota anayechezanchini Morocco katik klabu ya Wydad Casablanca Simon Msuva dakika ya 6 ya mchezo.

Katika mchezo huo golikipa Aishi Manula amefanya kazi ya ziada kuhakikisha Stars inaondoka na alama tatu baada ya kuokoa michomo ya hatari iliyofanywa na washambuliaji wa Benin.

Kwa ushindi huo Stars ipo kileleni mwa kundi J, wakiwa na alama 7 baada ya kucheza michezo minne sawa sawa na Benin.

Rais wa TFF Walace Karia aliongozana na Stars nchini Benin kama sehemu ya kuhamsisha ushindi kwa Stars.

Mchezo mwingine katika kubdi hilo utawakutanisha Madagascar dhidi ya DR Congoo.