Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 10 09Article 562330

Soccer News of Saturday, 9 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Stars yapania kufanya kweli Benin (+video)

Mwalimu Kim Poulsen akitoa maelekezo kwa wachezaji play videoMwalimu Kim Poulsen akitoa maelekezo kwa wachezaji

Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Kim Poulsen Taifa Stars amesema kuwa wanatambua kesho watakuwa na kazi ngumu mbele ya Benin ila wapo tayari kiakili na kimwili kwa mapambano.

Kim amesema anaamini kwamba utakuwa mchezo wa wazi na mzuri kwa kuwa wamejipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi na hicho ndicho kipaumbele cha kwanza.

Katika mchezo wa awali Stars ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Mkapa.Pia wachezaji leo wakiwa nchini Benin walifanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wa kesho.