Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2022 01 14Article 585916

Soccer News of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Stevie G Kuwavaa United Na Silaha mbili Mpya!

Mmoja miongoni mwa usajili mpya ndani ya Aston Villa, Coutinho Mmoja miongoni mwa usajili mpya ndani ya Aston Villa, Coutinho

Waswahili husema, “malipo ni hapahapa duniani”. Kwenye soka ni vivyo hivyo, malipo ni uwanjani. Stevie G uso na uso na Ralf Rangnick kwa mara ya pili wiki hii.

Aston Villa watakua Villa Park watakapowaalika Manchester United wikiendi hii. Baada ya kuambulia kipigo mapema wiki hii kule Old Trafford, hii ni fursa kwa Steven Gerard kulipa kisasi kama itawezekana.

United walishinda 1-0 dhidi ya Villa na kuwaondoa kwenye mashindano ya FA. Safari hii wanakutana kwenye muendelezo wa EPL. Huu ni mchezo wa namna ya kipekee, United anahitaji pointi 3 muhimu na Villa nao ni hivyohivyo.

Utofauti ni kwamba, Stevie G ameongeza silaha 2 mpya kwenye kikosi chake. Uwepo wa Philippe Coutinho na Lucas Digne, unamuongezea nguvu na hamasa Gerard kwenye mchezo huu.

Wachezaji wote wawili wameshajiunga na wachezaji wenzao kwenye vipindi kadhaa vya mazoezi, Stevie G anauhakika wa kuwatumia dhidi ya United endapo atahitaji kufanya hivyo. United ni ileile, anapungua Luke Shaw na Scot McTominay ambao wanatumikia adhabu ya kukosa mechi 1 kila mmoja.

Kukosekana kwa John McGinn kwa sababu kama za wachezaji wawili wa United, kunaweza kuwa fursa kwa Coutinho kuanza mchezo huu dhidi ya United.