Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 10 12Article 562699

Soccer News of Tuesday, 12 October 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

TETESI: Mrithi wa Saido Yanga Huyu Hapa

Mshambuliaji wa Uganda, Fahad Bayo Mshambuliaji wa Uganda, Fahad Bayo

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said Mohamed amesema kuwa kwa sasa mpango mkakati wao kama GSM ni kuhakikisha wanaimarisha kikosi cha Yanga ili kiwe imara kila idara kufanya vyema kwenye mashindano ya kimataifa msimu ujao.

Lakini pia, zipo taarifa ambazo bado hazijawekwa wazi kuwa mshambuliaji wa Yanga ambaye ni raia wa Burundi, Said Ntibanzonkiza ‘Saido’ kuna uwezekano kwenye dirisha dogo la usajiri ataachwa na mabosi wake hao.

Tetesi hizo zinadai kwamba nafasi yake inatajwa kuchukuliwa na mshambuliaji hatari na tegemeo kwa sasa wa timu ya taifa ya Uganda ambaye anakipiga katika Klabu ya Fc Ashdod ya Ligi Kuu Israel.

Mwamba huyu anafahamika kama Fahad Bayo ambaye alizaliwa 10 mei 1998 katika mji wa Lugazi Uganda.