Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 11 22Article 573325

Soccer News of Monday, 22 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Tanzania yamaliza kwa Kichapo COSAFA, yaambulia nafasi ya pili

Timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni Timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni

Timu ya Taifa ya Tanzania ya ufukweni, jana imemaliza nafasi ya pili kwenye michuano ya Soka la Ufukweni baada ya kufungwa 3-1 na Msumbiji katika Fainali ufukwe wa South Beach Arena Jijini Durban.

Ushindi huo ni mwendelezo wa ubabe wa Msumbiji kwa Tanzania, kwani mechi ya Kundi B walishinda kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 4-4.

Mechi nyingine Tanzania iliyo chini ya kocha Boniphace Pawasa ilishinda 3-1 dhidi ya Comoro Kundi A kabla ya kuifunga Angola 5-2 kwenye Nusu Fainali.