Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 10 13Article 562963

Soccer News of Wednesday, 13 October 2021

Chanzo: BBC Sports

Tetesi za Soka Ulaya 13.10.2021: Haaland, Sterling, Oxlade-Chamberlain, Dembele, Foden, Lenglet

Mshambuliaji wa Dortmund, Erling Braut Haaland Mshambuliaji wa Dortmund, Erling Braut Haaland

Wakala wa Erling Braut Haaland, Mino Raiola anatarajiwa kufanya mazungumzo na Manchester City kuhusu uwezekano wa uhamisho wa mshambuliaji huyo wa miaka 21 wa Borussia Dortmund na Norway msimu wa joto. (Times, subscription required)

Mshambuliaji wa England Raheem Sterling, 26, anataka kuhakikishiwa kwamba ni sehemu muhimu ya mipango ya Pep Guardiola kabla ya kuanza tena mazungumzo ya mkataba na Manchester City. (Sun)

Liverpool wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa England Alex Oxlade-Chamberlain, 28, - lakini kwa bei stahiki - huku klabu yake ya zamani ya Arsenal ikimtaka. (Mirror)

The Reds pia wameanza majadiliano ya kumsaini mshambuliaji wa Barcelona Mfaransa Ousmane Dembele, 24, kwa uhamisho wa bure msimu huu wa joto. (Mail, via Mundo Deportivo)

Kiungo wa kati wa England Phil Foden, 21, anakaribia kutia saini mkataba mpya Manchester City. Mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2024. (The Athletic, subscription required)

Manchester United wameungana na Chelsea na Juventus katika mbio za kumsaka kiungo wakati wa Monaco na Ufaransa Aurelien Tchouameni, 21. (Express)

Mlinzi wa Barcelona Clement Lenglet, 26, huenda akawa wa kwanza kuwasili Newcastle baada ya klabu hiyo kununuliwa hivi kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa akisemekana kuwa mchezaji klabu hiyo inamtaka. (Sport.es)

Wachezaji wa Southampton wanatarajia kocha wao Ralph Hasenhuttl, 54, atafutwa katika wiki chache zijazo hata. Kabla ya klabu hiyo kushinda taji ya Ligi ya Primia msimu huu. (Football Insider)

Mchezaji wa Uhispania Hector Bellerin, 26, amedokeza kwamba hana nia ya kurejea Arsenal mkataba wake wa mkopo wa msimu mzima Real Betis utakapokamilika. (El Desmarque, via Mail)

Beki wa Ujerumani Antonio Rudiger, 28, anatathmini hali ilivyo kabla ya kufanya uamuzi juu ya mustakabali wake katika klabu ya Chelsea, huku mkataba wake wa sasa ukitarajiwa kumalizika mwisho wa msimu. (Sky Sports)

Southampton,Tottenham na West Ham wanataka kumsaini kipa wa West Brom na England Sam Johnstone, 28. (Hampshire Live)

Real Madrid wanapania kumrudisha mlinzi wa Tottenham Mhispania Sergio Reguilon, 24, katika uwanja wa Bernabeu kabla ya msimu ujao. (Defensa Central, via Express)

Leeds United wanakaribia kumsajili mshambuliaji kinda wa Espanyol Mhispania Mateo Joseph Fernandez 17. Leeds wamewasilisha dau la pauni laki 450,000 lakini Espanyol wanataka pauni milioni moja (£1m). (Team Talk)