Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 10 11Article 562492

Soccer News of Monday, 11 October 2021

Chanzo: BBC Sports

Tetesi za soka Ulaya 11.10.2021: Haaland, Neymar, Sterling, Gerrard, Verratti, Morata, Traore

Wachezaji wa New Castle United Wachezaji wa New Castle United

Newcastle United itawalenga wachezaji wanne wa Manchester United wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa mwezi Januari huku mashambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 25, kiungo wa kati wa Uholanzi Donny van de Beek, 24, Beki wa Ivory Coast Eric Bailly na mshambuliaji wa England Jesse Lingard, 28, wote wakiwa katika orodha yao. (Mirror)

Wamiliki wapya wa klabu ya Newcastle United wana mpango wa kumbadilisha mkufunzi wa klabu hiyo na yule wa klabu ya Leicester City Brendan Rodgers. Mkufunzi wa klabu ya Rangers Steven Gerrard au aliyekuwa mkufunzi wa klabu ya Borussia Dortmund Lucien Favre. (Mail)

Aliyekuwa mkufunzi wa klabu ya RB Leipzig Ralf Rangnick pia ananyatiwa na Newcastle ili kuchukua wadhfa wa mkurugenzi wa michezo. (Telegraph - subscription required)

Naibu makamu wa rais wa klabu ya Barcelona Rafael Yuste amepuuza fursa ya klabu hiyo ya Uhispania kumsajili mshambuliaji hatari wa Borussia Dortmund raia wa Norway Erling Braut Haaland ,21 msimu ujao.. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Mshambuliaji wa Brazil Neymar, 29, amesema kwamba huenda kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar likawa lake la mwisho , kwa kuwa mshambuliaji huyo wa PSG hana uhakika iwapo akili yake ina uwezo wa kukabiliana na changamoto za kandanda. ". (DAZN, via Goal)

Barcelona huenda ikamuuza winga wa Ufaransa Ousmane Dembele iwapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 hatoongeza kandarasi yake nao na huenda klabu hiyo ya Uhispania ikajaribu kumsaini mshambuliaji wa Manchester City na England Raheem Sterling 26 kuchukua mahala pake. (Sport - in Spanish)

Juventus itamtumia kiungo wa kati wa Wales Aaron Ramsey, 30, kama chambo cha kumvutia kiungo wa kati wa Manchester United na nyota wa Ufaransa Paul Pogba, 28, kurudi mjini Turin. (Mail)

Tottenham inahusishwa na jaribio la kutaka kumsaini kiungo wa kati wa Marekani Weston McKennie, 23, na mchezaji wa Uswidi mwenye umri wa miaka 21 Dejan Kulusevski kutoka Juventus. (Calciomercato, via Teamtalk)

Tottenham inamnyatia mshambuliaji wa Uhispania mwenye umri wa miaka 28 Alvaro Morata kuchukua mahala pake Harry Kane, 28. Morata kwasasa yuko Juventus kwa mkopo kutoka Atketico Madrid (Fichajes - in Spanish)

Liverpool iko tayari kuwasilisha ombi lao la kumsajili winga wa Wolves na Uhispania Adama Traore, 25. (El Nacional - in Catalan)

Chelsea imekubali kuandikisha kandarasi mpya na kiungo wa kati wa Denmark Andreas Christensen,huku makubaliano hayo yakiendelea kukamilishwa kabla ya kutangazwa rasmi. (Fabrizio Romano on Twitter)

Kiungo wakati wa Itali Marco Verratti, 28, anasema kwamba analenga kuhudumu kipindi chote kilichosalia katika klabu ya Ufaransa ya PSG. (France Info - in French)