Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 10 12Article 562705

Soccer News of Tuesday, 12 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Twiga Stars yawasili nchini, Kocha azungumza

Wachezaji wa Twiga Stars wakiwasili Uwanja wa JNIA Wachezaji wa Twiga Stars wakiwasili Uwanja wa JNIA

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Wanawake "Twiga Stars" kimewasili nchini kikitokea Afrika ya Kusini ilipokwenda kushiriki Mashindano ya COSAFA WOMEN 2021 CHAMPIONSHIP.

Kikosi cha Twiga Stars kiliibuka bingwa baada ya kuichapa Timu ya Malawi katika mchezo wa fainali.

Katika michuano hiyo, nahodha wa Timu ya Taifa ya Wanawake “Twiga Stars” Amina Bilali amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano.