Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 11 22Article 573373

Soccer News of Monday, 22 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Ugeni wambeba Pablo kwa Ruvu

Pablo Franco , Kocha mpya wa Simba SC Pablo Franco , Kocha mpya wa Simba SC

Ugeni wa Kocha mpya wa Simba SC,imekua chachu ya mafanikio ya kuondoka na alama tatu katika mechi yake ya kwanza tangu achukue majukumu ndani ya kikosi hicho.

Haikuwa rahisi kwa benchi la ufundi la Ruvu Shooting kujua mfumo na mbinu anazotumia pablo hivyo iliwapasa kwenda kwa nadharia tu katika mechi ambayo waliishia kupokea kipigo cha mabao 3-1.

Bila shaka itakua ngumu kwa wapinzani siku za hivi karibuni kuenda kupambana na Simba huku wakijua namna ya kuwadhibiti kutokana na kutopata nafasi ya kumsoma Pablo mbinu zake.

Pengine labda baada ya michezo kadhaa wapinzani wakishaina Simba mfumo inaoutumia katika mechi zake watapata mbinu za kupambana nae.