Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2022 01 13Article 585532

Soccer News of Thursday, 13 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Wachezaji wanusurika kifo katika ajali ya Basi

Wachezaji wa Kalumbila FC wakijinasua katika ajali Wachezaji wa Kalumbila FC wakijinasua katika ajali

Timu ya Quattro Kalumbila FC inashiriki Ligi daraja la kwanza nchini Zambia imepata ajali asubuhi ya leo January 13, 2022 baada ya basi lao kuacha njia na kuanguka katika barabara ya Kapiri-Kabwe wakiwa njiani kuelekea Livingstone kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya Livingstone Pirates.

Chama cha Soka cha Zambia (FAZ) imethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema "Watu wawili wamejeruhiwa na hakuna kifo". Pia FAZ imeahirisha mchezo wa Daraja la Kwanza kati ya Livingstone Pirates na Quattro Kalumbila FC hadi tarehe itakayopagwa.