Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2022 01 11Article 585028

Soccer News of Tuesday, 11 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Wakala wa Dembele amuwashia moto Xavi

Ousmane Dembele Ousmane Dembele

Wakala wa nyota Ousmane Dembele amemchana kocha wa Barcelona Xavi Hernandez kuwa anashindwa kuwasimamia vyema wachezaji wake.

Suala la Dembele limekuwa zito kidogo akiwa amekwama kwenye suala la mazungumzo ya mkataba, mazungumzo ambayo yanaenda taratibu sana.

Inafahamika kuwa staa huyu anataka kusalia Barcelona, lakini anataka maboresho katika vipengele vya mkataba japokuwa Barcelona wapo katika changamoto ya kiuchumi.

Hiyo ina maana Dembélé anaweza kuongezewa mkataba wenye upungufu wa marupurupu ya sasa, na hiyo ndiyo sababu inayotajwa zaidi kusababisha mvutano wa sasa wa mkataba kati ya Barca na winga huyo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa wakala wa Dembélé, Moussa Sissoko, suala sio pesa.

Sissoko amenukuliwa akisema “Anaongea juu ya mengi lakini si suala la pesa. Ni suala la siku hadi siku. Usimamizi huu wa michezo, unafanya kazi bila kufanya mafunzo baada ya kutoka kwenye changamoto ya covid, ni ngumu kuelewa.”