Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 11 23Article 573754

Soccer News of Tuesday, 23 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Wakati tukiisikitikia Mtibwa, isisahaulike Azam

Azam FC mchezo wake wa mwisho ilipoteza dhidi ya KMC Azam FC mchezo wake wa mwisho ilipoteza dhidi ya KMC

Timu ya Mtibwa Sugar kutoka kule Manungu Mkoani Morogoro wakiwa hawajashinda mechi hata moja mpaka sasa ambapo Ligi Kuu imeshatamatisha raundi ya sita kwa kila timu.

Wengi wanaonesha kuwa na wasi wasi na mwennendo wa timu ya Mtibwa kwa sasa ikizingatiwa wana Kocha mwenye CV kubwa nchi ni akiwa ashafanikiwa kubeba ubingwa wa Ligi Kuu akiwa na Azam FC, Mcameroon Josph Omog.

Misimu miwili iliyopita Mtibwa imeponea chupu chupu kushuka daraja wakati msimu uliopita 2020/2021 iliwabidi kucheza michezo ya Play off kuendelea kubaki Ligi Kuu.

Wakati hayo yakijiri kwa upande wa Mtibwa, kuna Azam FC ambao wao wana kila kitu cha kuhakikisha wanapambania ubingwa wa Ligi Kuu kila msimu sambamba na Vigogo Simba na Yanga.

Azam FC matokeo yao katika mechi za Ligi Kuu hayaridhishi kwa sasa licha ya uwekezaji mkubwa unaofanyika, walimu bora nk.

Mashabiki na wapenzi wa Azam hawafurahishwi na mwenendo wa Timu hiyo na wanalalamikia benchi la ufundi kila kukicha kwa kuona wameshindwa kuwa na mbinu za kuifanya Azam kuwa tishio. Azam wana Kocha George Lwandamina.

Sasa kocha msaidizi wa timu ya Azam FC, Vivier Bahati, amesema kuwa hajafurahishwa na matokeo waliyopata baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa KMC, wameyaona mapungufu ya kikosi chao na wanaenda kuyafanyia kazi ili yasijirudie katika michezo ijayo.

Huu unakuwa mchezo wa tatu kwa Azam kupoteza msimu huu, ambapo ilifungwa mabao 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania baadaye 2-0 mbele ya vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga na juzi wamepoteza kwa KMC.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Bahati alisema kuwa hana sababu ya moja kwa moja kwanini wamepata matokeo hayo, wamepoteza mchezo mbele ya KMC kutokana na kukosekana kwa umakini katika baadhi ya maeneo yaliyowagharimu na kupoteza pointi tatu.

“Tumepoteza mchezo dhidi ya KMC, ulikuwa mchezo mzuri tuliingia uwanjani tukiwa na muendelezo mzuri wa matokeo, jambo ambalo lilitupatia matumaini ya kupata ushindi, lakini wapinzani wetu walikuwa bora zaidi yetu.

“KMC ni timu nzuri licha ya kwamba ilikuwa haipati matokeo mazuri katika michezo yao iliyopita tunapaswa kuwa makini katika mchezo ujao hasa katika eneo la ulinzi ambalo lilifanya baadhi ya makosa yaliyotuhukumu,” alisema Bahati.

Naye kocha msaidizi wa KMC, Habib Kondo alisema kuwa anafuraha kwa kupata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu msimu huu tena mbele ya timu bora, ingawa walifanya kazi ya ziada kuhakikisha pointi tatu zinabaki nyumbani, anaamini kuwa baada ya matokeo haya mambo yataanza kwenda vizuri.

“Dakika 15 za kwanza tuliingia tukijua nini tunaenda kufanya ndio maana tulipata bao dakika ya 12, najua sasa tutakuwa na vita kubwa ya kupata matokeo, lakini tumejipanga kuhakikisha tunaendelea kufanya vizuri zaidi.

“Tuliingia uwanjani tukiwa na tatizo kubwa la kisaikolojia kutokana na matokeo yetu tangu mwanzo wa msimu, ligi yetu mwaka huu ina presha kubwa, nashukuru tumeanza vizuri nyumbani tunaendelea kujipanga kwa ajili ya michezo inayofuata,” alisema Kondo.