Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 09 11Article 556903

Soccer News of Saturday, 11 September 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Watanzania 10 kibaruani CAF

Watanzania 10 kibaruani CAF Watanzania 10 kibaruani CAF

Maofisa 10 kutoka Tanzania, wameteuliwa kuwa wasimamizi wa mechi za awali za mashindano ya klabu Afrika zitakazochezwa katika miji na nchi tofauti barani Afrika

Uteuzi wa maofisa hao umefanywa na  idara ya afya na ile ya waamuzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ukihusisha waamuzi wa soka nane na maofisa wengine wawili ambao watakuwa na majukumu ya kusimamia mechi za Ligi ya mabingwa Afrika na zile za Kombe la Shirikisho Afrika zitakazochezwa kuanzia leo hadi Jumapili.

Waamuzi nane ambao wameteuliwa kuchezesha mechi za mashindano ya Klabu Afrika mwishoni mwa wiki hii ni Elly Sasii, Ramadhan Kayoko, Kassim Mpanga, Martin Saanya wao wameteuliwa kuchezezesha mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika baina ya URA ya Uganda na Coffee ya Ethiopia utakaochezwa kwenye Uwanja wa St. Mary's, Kampala Uganda, Septemba 12.

Katika mchezo huo ambao URA watakuwa wenyeji, Sasii atakuwa refa wa kati ambapo atasaidiwa na washika vibendera Mohamed Mkono na Kassim Mpanga huku Saanya akipangwa kuwa mwamuzi wa akiba.

Refa Ramadhan Kayoko yeye amepangwa kuchezesha mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya Mogadishu City ya Somalia na APR ya Rwanda utakaochezwa keshokutwa Jumapili huko Djibouti, City Djibouti na atasaidiwa na refa msaidizi namba moja, Frank Komba na msaidizi mwingine akiwa ni Soud Lila na refa wa akiba akiwa ni Mfaume nassoro.

Ukiondoa majukumu hayo kwa waamuzi, Watanzania wengine, Violet Lupondo na Hamid Abdallah Masoud wao wameteuliwa kuwa wasimamizi wa vipimo vya Ugonjwa wa Uviko-19 kwa mechi zitakazochezwa hapa nchini.

Wakati Lupondo akiwa Ofisa wa CAF wa vipimo vya Uviko kwa mechi baina ya Azam na Horseed na ila ya Yanga na Rivers United, Masoud yeye ameteuliwa kuwa ofisa msimamizi wa vipimo hivyo kwa mechi baina ya KMKM na Al Ittihad na ile baina ya Mafunzo na InterClube