Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2022 01 14Article 585898

Soccer News of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Xavi Kumtoa kwa Mkopo Depay

Kocha wa Barca havutiwi na Memphis Depay Kocha wa Barca havutiwi na Memphis Depay

Kocha wa klabu ya Barcelona Xavi Hernandez, yupo kwenye mikakati ya kumpeleka kwa mkopo nyota wa timu hiyo Memphis Depay wa miezi sita ili kuweza kumpa nafasi ya kucheza mholanzi mwenzie Luuk de Jong.

Mshambuliaji wa uholanzi Memphis Depay amekuwa na msimu mzuri kwenye klabu ya Barcelona huku akiweza kufunga mara 8 kwenye michezo 16 kwenye La Liga, lakini hajaweza kumshawiahi kocha wake aliyetua novemba akichukua mikoba ya Ronald Koeman.

Xavi amekuwa akivutiwa zaidi na mchezji wa kimatifa kutoka uholanzi ambaye anatokea taifa moja na Depay, huku wiki za karibuni aamekuwa akimtumia zaidi .

Kwenye mchezo wa El Clasico Depay alianzia benchi huku De Jong akiwa kwenye kikosi, huku mchezo wake wa kwanza dhidi ya mallorca mwaka huu 2022 aliweza kufunga huku siku sita baadae alifunga tena dhidi ya Granada