Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 11 21Article 573301

Soccer News of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Xavi: Sina uhakika na kustaafu kwa Aguero

Meneja wa Barcelona, Xavi Hernandez Meneja wa Barcelona, Xavi Hernandez

Meneja wa timu ya Barcelona, Xavi Hernandez amesema hana uhakika na kustaafu kwa mshambuliaji wake Kun Aguero na kusema hakuna uhakika huo.

Aguero hivi karibuni kulizuka tetesi ya kuwa anataka kustaafu kutokana na matatizo ya moyo aliyonayo baada ya kushindwa kumaliza mechi dhidi ya Alaves, ambayo ndio tatizo lilionekana na kukimbizwa hospitalini haraka kwa ajili ya vipimo zaidi.

"Sijui kitu chochote, nilizungumza nae na hicho kinachosambaa si cha kweli, sisi hatuna hizo taarifa na sijui zimetokea wapi, nimemwambia arudi atakopojisikia vizuri, na tutakapo pata taarifa sahihi za daktari" amesema Xavi

Kun Aguero anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa miezi mitatu kwa ajili ya uchunguzi na uangalizi zaidi wa afya yake na hatma yake itajulikana baada ya madaktari kuthibitisha kama hataweza kuendelea na kazi yake hiyo.

Xavi jana aliiongoza klabu ya Barcelona kwenye mchezo wake wakwanza na kupata ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Espanyol na huku goli pekee la likifungwa na Depay kwa mkwaju wa penati dakika ya 48.