Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 09 13Article 557227

Soccer News of Monday, 13 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Yanga mna deni kwa Molinga

David Molinga, Mshambuliaji wa Namungo David Molinga, Mshambuliaji wa Namungo

Straika mpya wa Kikosi cha Namungo, David Molinga ametaka mabeki wa timu pinzani kujiandaa vya kutosha kukabiliana nae na hususani waajiri wake wa zamani klabu ya Yanga, ambao waliachana nae.

Molinga ni miongoni mwa sajili bora na za kimkakati zinazoendelea kufanywa na timu za Ligi kuu kuelekea Msimu wa 2021/02022. Kutokana na kamba nyakati za nyuma wachezaji kama hawa walikuwa na nafasi ya kucheza Simba, Yanga ama Azam.

Molinga ama "Falcao" kama anavyojulikana na wengi alikamilisha usajili wake wa kujiunga na Namungo na kutangazwa rasmi Septema 1, mwaka huu akitokea kwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Zambia klabu ya Zesco United, aliyoichezea msimu uliopita.

Molinga ameshawahi kuhudumu katika Klabu ya Yanga msimu wa 2019/2020 kable ya kuachwa na wanajangwani hao.

“Ni jambo zuri kwangu kurejea tena na kucheza soka Tanzania, kwangu nchi hii ni kama nyumbani kwangu na nimefarijika sana kujiunga na Namungo. Deni kubwa ambalo ninalo ni kuhakikisha naonyesha uwezo mkubwa na kuwathibitishia viongozi wa Namungo kuwa hawakukosea kuniamini".

“Natarajia msimu ujao utakuwa mgumu kutokana na maandalizi ya kila timu ikiwemo suala la usajili, lakini kama mchezaji nimejipanga kuhakikisha nafanya vizuri kwenye kila mchezo hususani pale nitakapokutana dhidi ya waajiri wangu wa zamani Yanga,”

Timu ya Namungo itafungua pazia la Ligi kuu dhidi ya wageni Geita Gold Septemba 27 Mkoani Lindi.