Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 09 13Article 557260

Soccer News of Monday, 13 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Yanga yasukwa kimya kimya

Godfred Nyarko Godfred Nyarko

Baada ya kutulia kwa takribani majuma matatu sasa, wanajagwani wanatajwa kushusha kifaa kingine kutoka Medeama FC, kuonesha ni kweli wamepania kufanya jambo msimu ujao.

Mpaka hivi sasa, Yanga imebakisha nafasi mbili za wachezaji wa kimataifa ambayo tayari ina kumi pekee ambao ni kipa Djigui Diarra, Klahid Aucho, Jesus Moloko Mukoko Tonombe, Yacuoba Songne, Yannick Litombo, Said Ntibanzonkiza ‘Saido”, Shaban Djuma na Heritier Makambo.

Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika kiungo Godfred Nyarko yupo nchini zaidi ya wiki moja akiendelea kuangaliwa na kocha mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi huko kambini Kijiji cha Avic Town, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Na taarifa zinasema huenda akawa sehemu ya kikosi cha Yanga kwa kuwa mpaka hivi sasa ameshaonesha kiwango kikubwa akiwa mazoezini katika kamboi ya Yanga huko Kigamboni.

Kiungo huyo atasajiliwa katika dirisha dogo msimu huu baada ya benchi la ufundi na uongozi kukubali uwezo wake katika mazoezi ya timu hiyo.

Yanga ina kila sababu ya Kujaza nafasi mbili zilizobaki hasa baada ya Wachezaji wake watatu, beki Djuma Shaban, Kiungo Khalid Aucho na Straika Fiston Mayele kuzuiliwa kucheza Michuano ya klabu bingwa Afrika na bado haijajulikana sakata lao litakwisha lini.