Uko hapa: NyumbaniMichezoTennis2022 01 14Article 585817

Tennis News of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Australia Yafuta tena VISA ya Djokovic

Mcheza Tennis, Novac Djokovic Mcheza Tennis, Novac Djokovic

Serikali ya Australia imefuta tena kwa mara ya pili VISA ya mchezji bora wa Tennis duniani, Novak Djokovic na anakabiliwa na kufukuzwa nchini humo kabla ya mashindano ya Australian Open.

Uamuzi huo ulikuwa unasubiriwa tangu jaji alipobatilisha uamuzi wa awali siku ya Jumatatu ili kujua kama Waziri wa Uhamiaji Alex Hawke atatumia mamlaka yake kurejesha adhabu hiyo.

Kabla ya saa kumi na mbili jioni saa za Australia siku ya Ijumaa, Hawke alitoa taarifa akisema alikuwa amefanya uamuzi wa kumrudisha Djokovic nyumbani kwa misingi ya afya na utaratibu mzuri.

“Leo nilitumia mamlaka yangu chini ya kifungu cha 133C(3) cha Sheria ya Uhamiaji kufuta visa aliyokuwa nayo Bw Novak Djokovic kwa misingi ya afya na utaratibu mzuri, kwamba ilikuwa ni kwa manufaa ya umma kufanya hivyo.” alianza Hawke.

“Uamuzi huo ulifuata maagizo ya Mahakama ya Shirikisho na Familia mnamo tarehe 10 Januari 2022, ikibatilisha uamuzi wa awali wa kughairiwa kwa misingi ya haki ya kitaratibu.

“Katika kufanya uamuzi huu, nilizingatia kwa uangalifu habari niliyopewa na Idara ya Mambo ya Ndani, Jeshi la Mipaka la Australia na Bw Djokovic.

“Serikali ya Morrison imejitolea sana kulinda mipaka ya Australia, haswa kuhusiana na janga la COVID-19.” aliongeza Hawke.

Habari hiyo mbaya kwa Djokovic imekuja ikiwa mashindano ya Australian Open yakitaraji wa kuanza Jumatatu ya wiki ijayo, na taarifa hiyo inaonyesha wazi mchezaji huyo atakosa mashindano hayo.