Uko hapa: NyumbaniMichezoTennis2022 01 13Article 585469

Tennis News of Thursday, 13 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Djokovic Kuanza na Kecmanovic Australian Open

Mcheza Tennis, Novac Djokovic Mcheza Tennis, Novac Djokovic

Mcheza Tennis namba moja kwa ubora duniani, Novak Djokovic amesalia kwenye droo ya michuano ya wazi ya Australian Open huku kukiwa hakuna taarifa kamili kama atacheza michuano hiyo.

Katika droo iliyofanyika bingwa huyo mara tisa amepangwa dhidi ya Mserbia mwenzake Miomir Kecmanovic.

Wakati huo bingwa wa Uingereza wa US Open Emma Raducanu, anayeshika namba 17 duniani atachuana na mchezaji namba 68 wa Amerika Sloane Stephens, bingwa wa 2017 kwenye mashindano ya New York.

Australian Open ndiyo Grand Slam ya kwanza msimu wa 2022 na itaanza Melbourne Park Jumatatu ya wiki ijayo.

Djokovic, 34 alifanya mazoezi tena Melbourne Park mapema Alhamisi, huku waziri wa uhamiaji wa Australia Alex Hawke bado hajaamua kama atabatilisha visa yake tena na kumuondoa nje ya nchi.

Djokovic ana matumaini ya kushinda taji la 10 la Australian Open lililoongeza rekodi ambalo litakuwa taji lake la 21 la Grand Slam, na kuwaondoa Roger Federer wa Uswizi na Rafael Nadal wa Uhispania.

Djokovic hana chanjo ya Covid-19 na visa yake ilifutwa alipofika Australia wiki iliyopita, kufuatia maswali juu ya kutopokea chanjo ambayo ingemruhusu kuingia.

Hata hivyo, siku ya Jumatatu hakimu alibatilisha uamuzi huo kwa kiasi kikubwa na kuamuru mchezaji huyo aachiliwe kutoka katika hoteli inayozuia wahamiaji.

Siku ya Jumatano, Djokovic alikiri kukutana na mwandishi wa habari wa L’Equipe mnamo Disemba 18 licha ya kujua alipimwa na kukutwa na Covid, na vile vile kulikuwa na makosa kwenye fomu zake za uhamiaji.