Uko hapa: NyumbaniMichezoTennis2022 01 13Article 585640

Tennis News of Thursday, 13 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Tsitsipas: Djokovic anawafanya Wachezaji waonekane Wajinga

Stefanos Tsitsipas Stefanos Tsitsipas

Mchezaji namba nne kwa ubora duniani Stefanos Tsitsipas amemshutumu mchezaji namba moja kwa ubora duniani Djokovic kwa kuwafanya wachezaji wengine wa tennis kuonekana wajinga baada ya kuruhusu kucheza pasipo kuchanjwa.

Tsitsipas hakubaliani na wenzie ambao waliweza kusimama kuweza kumtetea Djokovic ili aweze kupewa ruhusu ya kuweza kushiriki hata kama hajachanja ili aweze kutetea na kuhakikisha anachukua ubingwa 10 Australian Open huku akihakikisha anachukua Grand Slam ya 21.

Tsitsipas ambaye mwaka jana alipoteza fainali ya French Open, alisema kuwa karibia wahiriki wote wamechanjwa kwenye mashindano hayo ambayo yanakwenda kufanyika jijini Melbourne

“Amechagua kufuata njia yake ambayo inawafanya wengine waonekane wapumbavu, ni uthubutu mkubwa ambao wamefanya kuiweka Grand Slam kwenye hatari, sidhani kama wachezaji wengi wangefanya hivyo.” Alisema Stefanos Tsitsipas

waziri mkuu wa Australia Scott Morrison alisema kuwa hakuna jambo lilifanyika la kufuta VISA yake kwa mara ya pili, Djokovic hakuweza kuhusishwa kwenye mzunguko wa kwanza wa Australian Open.