Uko hapa: NyumbaniNchiPeopleSiasaAmina Chifupa

Watu Maarufu Tanzania

Siasa

Amina Chifupa

Amina Chifupa Mwanadada Shupavu

Amina Chifupa.jfif
Tarehe ya Kuzaliwa:
1981-05-20
Mahali pa Kuzaliwa:
NA
Date of Death:
2007-06-26
DECEASED

Amina Chifupa alizaliwa tarehe 20 Mei, mwaka 1981 na amefariki tarehe 26 Juni 2007. Chifupa alisoma shule ya msingi Ushindi na kujiunga na masomo ya sekondari Kisutu kabla ya kuingia shule nyingine ya sekondari ya Makongo alikomaliza elimu ya kidato cha sita mwaka wa 2001.

Kabla ya kumaliza masomo mwaka 1999, alianza kazi ya Utangazaji wa Kituo cha Redio cha Clouds FM cha Dar kilichokuwepo posta na aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Mama Shughuli.

Amina Chifupa alifariki akiwa na umri wa miaka 26 majira ya saa 3:00 katika Hospitali Kuu ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) Lugalo Dar es Salaam kwa maradhi ya mfadhaiko wa akili yaani “depression”.

Alikua ni mwanamke mpambanaji na mwanachama mahiri wa CCM. alipata nafasi mbalimbali za kukitumikia chama ,kuwa Kamanda wa CCM wa umoja wa Vijana katika tawi la Mikocheni A jijini Dar na amekuwa Katibu wa Kamati ya Uchumi ya UVCCM mkoa wa Dar, aliwahi kuwa Mama Mlezi wa UVCCM na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) matawi ya Bunju na Mbagala.

Mnamo Desember 28, 2005 Amina alipata nafasi ya kuteuliwa na serikali ya awamu ya nne kuwa Mbunge wa viti maalum kwa miaka mitano hadi Desemba 27,1010 namba yake ya usajili kama mbunge ikiwa ni 1313.

Amina alikuwa na upewo mkubwa na aliweza kujiamini sana japo kuwa umri wake ulikuwa mdogo aliweza kujenga hoja mbalimbali ndani na nje ya Bunge. Katika kipindi kifupi akiwa Mwanasiasa kijana, aliweza kusimama na kujipembua na wabunge wengine kwa kusimama kidete kupiga vita biashara ya mihadarati ambayo alaiamini inaua vijana ambao ni taifa l kesho.

Alijitoa muhanga na kusimama kidete kuafanya harakati za kupambana na wauzaji wa mmadawa za kulevya kwa kutoboa siri za wafanya biashara hao kuna wakati alipata kutishiwa maisha na kupelekea kupewa ulinzi kwa muda.

Amina alifariki akiwa na msuguano na baadhi ya viongozi wa UVCCM ambao walituhumiwa kumwona kuwa tishio katika nafasi ya uenyekiti wa Umoja huo ngazi ya Taifa.

Wakati mwili wake unatolewa hospitali ya Lugalo siku ya jumatano 27,2007 Maelfu ya wakazi wa Jijini Dar es Salaam na vitongoji vyake walifurika pembezoni mwa barabara za Bagamoyo na Kambarage wakiwa wameduwaa, wenye majonzi wakiupokea mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CCM Amina Chifupa.

hiyo ilikuwa ni ishara kubwa ilivyodhirisha kuwa Amina ni kipendi za watanzania wengi mchango wake katika siasi ulionekana kugusa watu wengi sana kwakuwa alikuwa akipaza sauti kukemea swala zima la vijana kuharibika na matumizi ya dawa za kulevya.

Amina chifupa Alizikwa majira ya saa 10 jioni ya Juni 28, 2007 kijijini Lupembe Wilayani Njombe mkoa wa Iringa.

TanzaniaWeb