Uko hapa: NyumbaniNchiPeopleSiasaAnna Mghwira

Watu Maarufu Tanzania

Siasa

Anna Mghwira

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro

Mgwira1
Tarehe ya Kuzaliwa:
1959-01-23
Mahali pa Kuzaliwa:
Tanzania
Date of Death:
2021-07-22
DECEASED

Anna, Elisha Mghwira, alizaliwa mnamo mwaka 1959, tarehe 23 mwezi januari katika kata ya Mungumaji iliyopo mkoa wa Singida na kufariki mwaka 2021, tarehe 22 mwzi Julai katika hospitali ya Mount Meru akiwa na umri wa miaka 62.

ELIMU

Alipata shahada ya Theolojia katika chuo kikuu cha Tumaini na baadae kujiungana chuo kikuu cha Dar es Salaam akichukua shahada ya Sheria mwaka 1986. Mwaka 2000, alitunukiwa shahda ya sheria katika chuo kikuu cha Essex kilichopo Uingereza.

SIASA.

kabla ya Umauti, alikuwa amekwisha staafu, kuhudumu kama Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

aliteulliwa na Hayati Magufuli kushika wadhifa huo mara baada ya kumaliza kushiriki wa uchaguzi mkuu wa Urais alipogombea nafasi ya Urais kwa tiketi ya chama cha ACT-WAZALENDO mwaka 2015.

Uteuzi huu uliwashtua watu wengi nchini na wengi walimuona kama msaliti lakini hizo ni siasa na siku zote siasa hazina mwenyewe.

Baada ya Uteuzi huu alihama kutoka ACT-WAZALENDO na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi CCM.

Lakini turudi nyuma kidogo, alianza siasa zake kipindi bado Tanganyika ipo chini ya TANU, aloihudumu kama kiongozi wa vijana kabla ya kuachia nafasi hiyo ili kuendelea na masomo yake.

Alirudi tena kwenye safu ya siasa na harakati, mwaka 2009, alipojiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

Alitupa Karata kuwania Ubunge katika jimbo la Arumeru ambapo alishindwa katika kura za maoni na Joshua Nasari, wakati huo huo alikwenda kushiriki katika bunge la Afrika Mashariki ambapo bahati haikuwa kwake tena.

Mwaka 2015 alihama kutoka chama cha CHADEMA, na kuhamia ACT-WAZALENDO alipokwenda kuwania Urais, na hapa ndipo watanzania walipo mjua kwa ukubwa Anna ni nani? mwanamke anagombea urais? haya yalikuwa ni mwaswali ya wengi.

Mwaka 2017, alihama kutoka ACT- WAZALENDO na kujiunga na Chama cha Mapinduxzi hadi umauti ulipomkuta.

TanzaniaWeb