Uko hapa: NyumbaniNchiPeopleWanadiplomasiaBalozi Ombeni Yohana Sefue

Watu Maarufu Tanzania

Wanadiplomasia

Balozi Ombeni Yohana Sefue

Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu

Amb Ombeni Sefue2
Tarehe ya Kuzaliwa:
1954-08-26
Mahali pa Kuzaliwa:
Tanzania

Balozi Ombeni Yohana Sefue Katibu Mkuu Kiongozi. Alizaliwa tarehe 26 Agosti 1954 wilayani Same mkoani Kilimanjaro. Alianza rasmi wadhifa wake tarehe 30 Desemba 2011.

Elimu.

Balozi Sefue alihitimu mafunzo ya shahada ya kwanza ya Utawala mwaka 1977 katika chuo kikuu cha Mzumbe Morogoro. Alipata Shahada ya pili ya uzamili katika sera na Utawala kutoka Taasisi ya Mafunzo Mitaala ya Jamii (ISS) huko The Hague, Uholanzi mwaka 1981. Pia ana stashada ya Juu katika uhusiano wa kimataifa na Diplomasia cha Tanzania - Msumbiji , Dar es salaam nchini Tanzania mwaka 1986.

Historia Fupi.

Balozi Ombeni Yohana Sefue alianza kazi ya kuwa balozi wa Tanzania nchini Marekani Juni 15 mwaka 2007. Kabla ya Uteuzi huo alikuwa balozi wa Tanzania nchini Kanada kuanzia Oktoba 2005 hadi Juni 2007. Pia alikuwa balozi mdogo wa Tanzania huko Stockholm nchini Sweden kati ya mwaka 1987 hadi 1992. Mwaka 1993 na 2005 alikuwa mwandishi wa hotuba na msaidizi binafsi wa Marais wa Tanzania - Rais Ali Hassan Mwinyi mwaka 1993-1995 na Rais Benjamini William Mkapa mwaka 1995-2005.

Miongoni mwa mambo mengine , Balozi Sefue alimsaidia Mkapa alipokuwa kwenye Tume ya Afrika (Tume ya Blair) iliyotoa ripoti yake ya "Maslahi yetu ya pamoja: Ripoti ya Tume ya Afrika Machi 2005 na alishiriki pamoja na Rais Mkapa katika mkutano wa nchi zinazoongoza kwa viwanda duniani (G8) uliojadili ripoti hiyo , Gleneagles, mwanzoni mwa mwezi Julai 2005.

Aidha alifanya kazi na Rais Mkapa alipokuwa mwenyekiti mwenza wa Tume ya Dunia ya ILO,kuhusu mwelekeo wa Jamii wa Utandawazi kati ya mwaka 2002 na 2004 katika kuandaa ripoti ya Tume hiyo Utandawazi usio na upendeleo: Kutoa Fursa kwa wote iliyotolewa Februari 2004. Katika kipindi cha takribani miaka 13 alichofanya kazi na marais wawili, Balozi Sefue alihusika na kazi za Umoja wa Mataifa, Umoja wa Nchi huru za Afrika , Jumuiya ya Madola, Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika mashariki (EAC). Amefanya kazi na Rais Mkapa kuhusu kuleta amani katika ukanda wa nchi za maziwa makuu, mkutano wa Uchumi Duniani Davos na Cape Town, Mkutano wa China na Afrika pamoja na TICAD.

Balozi Ombeni Yohana Sefue na mke wake, Anita wana watoto wawili wa kike (1989) na wa kiume (1990) .

Taarifa za Serikali