Uko hapa: NyumbaniNchiPeopleGovernment OfficialsBasil Mramba

Watu Maarufu Tanzania

Government Officials

Basil Mramba

Waziri wa Fedha na Uchumi

Basil Mramba
Tarehe ya Kuzaliwa:
1940-05-15
Mahali pa Kuzaliwa:
Tanzania
Date of Death:
2021-08-17
DECEASED

Basil Pesambili Miramba, ni mwanasiasa mashuhuri na nguli kuwahi kutokea hapa nchini, alikuwa ni mwanachama wa chama cha Mapinduzi na mbunge wa jimbo la Rombo, Kilimanjaro. Alizaliwa mnamo mwaka 1940 tarehe 15 ya mwezi wa 5.

Alipata elimu yake msingi katika shule ya Mkuu mission kwa darasa la kwanza na la tatu, kisha alirudi kijijini kwao rombo aliposoma shule ya mission ya kanisa katoliki kwa darsa la nne, na kurejea tena katika shule ya Mkuu Mission kwa ajili ya elimu zaidi.

Elimu yake ya juu aliipata katika chuo kikuu cha Makelele kilichopo nchini Uganda, alitamani sana kusoma sheria lakini ilimlazimu kusoma mambo ya utawala,alipiga hatua tena katika elimu alipoenda kusoma katika chuo kikuu cha mjini London alipochukua shahada ya uzamili katika biashara.

Safari yake ya Siasa ilianza mara moja tu alipomaliza elimu yake nchini Uganda, pale alipopewa agizo na Hayati Mwalimu Nyerere, kulisaidia taifa katika kutataua changamoto za viwanda, agizo lilimshtua kwa kuwa kwa wakati huo hakuwa mwanasiasa.

Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000 ulichora rasmi mstari wa siasa za mramba, alirejea Rombo kwa ajili ya kugombea ubunge, alishnda uwakilishi huo, huku kazi zake zikiwagusa sio tu watu wa Rombo bali wananchi wote wa Tanzania hasa pale alipoteuliwa kuwa Waziri wa fedha na uchumi chini ya uongozi wa Hayati Benjamini Mkapa.

Wakazi wa Rombo wanao msemo wao, wanasema huwezi kutaja maendeleo ya Rombo pasipo kumtaja Mramba, hakika hayauwa maneno bali ilithibitika katika uchaguzi mkuu wa 2005, alipochaguliwa tena kuwaongoza wananchi wa Rombo kwa mara nyingine.

Awamu hii aliteuliwa tena kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara kwa mwaka 2006-2008 kabla ya Baraza la Mawaziri kuvunjwa chini ya Uongozi wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete.

Katika kila safari kuna kupanda na shuka vivyo hivyo katika siasa, mwaka 2012, Mramba alifikishwa Mahakamani kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka akiwa Waziri wa Fedha na Uchumi,alishitakiwa pamoja na Waziri Nishati na Madini Daniel Yona kwa kuisababishia serikali hasara ya bilioni 11.7 kwa kutoa misamaha ya kodi isiyotakiwa.

Alihukumiwa mwaka 2015 kwenda jela miaka 3, kabla ya Mahakama kubadili kifungo ambapo Mramba na mwenzake walianza kutumikia kifungo cha nje kwa miezi 6 baada ya kukata rufaa kuomba kutumikia aina hiyo ya kifungo huku kigezo kikubwa kikiwa ni umri, ambapo kwa Sheria ya Huduma ya Jamii namba 6, inayosema mtu anayetiwa hatiani kwa kosa ambalo adhabu yake ni chini ya miaka tatu basi anaweza kutumikia kifungo cha nje.

Mramba litumikia kifungo cha nje katika hosptali ya Sinza Palestina. Utashi wake wa kutetea watu haukuzimwa na hukumu aliyopata, aliendelea kupaza sauti kwa wafungwa huku akiitaka serikali iwasaidie wafungwa kutumia taaluma zao, aliacha alama kila apokanyanga.

Baada ya kumaliza kifungo chake, alirejea katika maisha yake ya kawaida, nakuanzisha miradi ya maendeleo, alifungua Shirika binafsi la kusaidia na kutoa misaada kwa wahitaji.

Agosti 17 mwaka 2021, Mramba alifariki dunia katika hospitali ya Regency iliyopo jijini Dar es Salaam, kwa ugonjwa wa Uviko-19. Hakika alikuwa kiongozi mwenye uthubutu alama ya matendo yake itaishi daima katika taifa la Tanzania.

TanzaniaWeb