Uko hapa: NyumbaniNchiPeopleHeads of StateBenjamin William Mkapa

Tanzania Famous People

Heads of State

Benjamin William Mkapa

Rais Mstaafu

Mkapa 1
Date of Birth:
1938-11-12
Place of Birth:
Lupaso

Benjamini William Mkapa (12 Novemba 1938 - 24 Julai 2020) alikuwa Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1995-2005) na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, CCM.

Wasifu

Mkapa alizaliwa Lupaso karibu na Masasi katika kusini-mashariki ya Tanganyika. Kuanzia 1945 hadi 1951 alsoma shule za msingi pale Lupaso na Ndanda. 1952/53 alisoma shule ya seminari ya Kigonsera akaendelea kwenye shule ya sekondari ya watawa Wabenedikto pale Ndanda hadi kumaliza O-level. 1958/59 alimaliza A-levels pale St Farncis, Dar es Salaam (leo hii Pugu Secondary). Alipokelewa kwenye Chuo Kikuu cha Makerere alipohitimu 1962. Hatua za maisha ya kazi

Aprili 1962: Afisa tawala Dodoma Aprili 1962: Mkuu wa Wilaya Agosti 1962: alijiunga na Utumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje Mei 1966: Mhariri mkuu, gazeti la Uhuru Aprili 1972: Mhariri mkuu, Daily News Julai 1974: Afisa habari katika Ofisi ya Rais, Dar es Salaam Julai 1976: Mwanzilishi na mhariri mkuu wa Shirika la Habari Tanzania (SHIHATA) Oktoba 1976: Balozi wa Tanzania pale Nigeria Februari 1977: Waziri wa Mambo ya Wje Novemba 1980: Waziri wa Habari na Utamaduni Aprili 1982: Balozi wa Tanzania pale Kanada Februari 1983: Balozi wa Tanzania pale Marekani Aprili 1984: Waziri wa Mambo ya Nje 1990: Waziri wa Habari na Utangazaji Mei 1992: Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu Novemba 1995: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais wa Tanzania

Katika mwaka wa 1995, Mkapa alichaguliwa rais msingi wake ukiwa kampeni maarufu ya kupambana na ufisadi na kuuungwa mkono kwa nguvu na rais wa zamani Julius Nyerere. Juhudi za Mkapa za kupambana na ufisadi ni pamoja na kuumba jukwaa la wazi lililoitwa Tume ya Rais juu ya Ufisadi (Tume ya Warioba) na kuongeza msaada kwa Afisi ya Kuzuia Ufisadi.

Muhula wa pili wa miaka 5 wa Mkapa kama Rais uliisha Desemba 2005. Katika wakati wake ofisini, Mkapa alibinafsisha kampuni zilizomilikiwa na serikali akaweka sera za soko huria. Wafuasi wake walimtetea kuwa kuvutia uwekezaji wa kigeni ungesaidia kukuza uchumi. Sera zake zilipata msaada wa Benki ya Dunia na IMF na kupelekea baadhi ya madeni ya nje ya Tanzania kufutiliwa mbali.

Amekashifiwa kwa upungufu wa baadhi ya jitihada zake za kupambana na ufisadi vilevile matumizi mabaya ya fedha za umma. Utawala wake ulikuwa na matumizi sana na maposho bila kikomo. Alitumia £ 15 milioni kununua ndege ya binafsi ya kirais, vilevile karibu £ 30 milioni kwa vifaa vya angani vya kijeshi ambavyo wataalamu waliona yalizidi mahitaji machache ya majeshi ya nchi. Ilikuwa juu ya ununuzi huo wa mwisho ndipo Katibu wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza wa wakati huo Clare Short alielezea hasira ya umma, na kusababisha yeye kujulikana kama 'Mama Radar' katika vyombo vya habari vya Tanzania.

Baada ya kutoka ofisini kwa kukamilisha mihula miwili inayoruhusiwa, Mkapa alikumbwa na shutuma nyingi za ufisadi kati yao kujipa mwenyewe na Waziri wake wa zamani wa nishati na madini Daniel Yona "Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira" yenye faida kubwa katika Nyanda za juu za kusini mwa Tanzania bila taratibu zifuatazo. Kwa kujibinafsishia mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, alivunja katiba ya Tanzania ambayo haimruhusu rais kufanya biashara yoyote katika ikulu[onesha uthibitisho].

Aliteuliwa katika Bodi ya Wadhamini ya Chuo cha Aga Khan mwezi Novemba 2007.

Heshima na Tuzo Nishani Nishani Nchi Mwaka Ref Order of the Golden Heart of Kenya.svg Nishani ya Moyo wa Dhahabu wa Kenya (Chifu) Bendera ya Kenya Kenya 2005 Order of Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Tanzania) - ribbon bar.png Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Bendera ya Tanzania Tanzania 2011

Mnamo Desemba 7, 2019, alitunukiwa Nishani ya Heshima ikiwa ni kuthamini mchango wake katika kuanzisha vyuo vikuu binafsi, hivyo kukifanya Chuo Kikuu cha Iringa kuwa chuo kikuu cha kwanza binafsi nchini Tanzania wakati wa utawala wake. Shahada za Heshima Chuo Kikuu Nchi Shahada ya Uzamivu Mwaka Ref Chuo Kikuu cha S?ka Bendera ya Japani Japan Shahada ya Heshima 1998 Chuo cha Morehouse Flag of the United States.svg Marekani Shahada ya Heshima 1999 Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Bendera ya Tanzania Tanzania Shahada ya Heshima 2003 Chuo Kikuu ya Kitaifa cha Lesotho Bendera ya Lesotho Lesotho Daktari wa Sheria 2005 Chuo Kikuu cha Kenyatta Bendera ya Kenya Kenya Daktari wa Elimu 2005 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bendera ya Tanzania Tanzania Shahada ya Heshima 2005 Chuo Kikuu cha Nyukasal Flag of the United Kingdom.svg Ufalme wa Maungano Daktari wa Sheria ya Kiraia 2007 Chuo Kikuu cha Rasi ya Pwani (Cape Coast) Bendera ya Ghana Ghana Daktari wa Barua 2008 Chuo Kikuu cha Makerere Bendera ya Uganda Uganda Daktari wa Sheria 2009 Marejeo

"Benjamin Mkapa", Microsoft Encarta Encyclopedia 2001, WGBH (FM), pbs.org, ilitolewa 19-Oktoba-2009 JPM’s sentiments on Lupaso Road come true, gazeti la Daily News ya 27 Julai 2020, iliangaliwa Agosti 2020 Benjamin Mkapa, ABOUT President of Tanzania BENJAMIN WILLIAM MKAPA, tovuti ya dsctanzia.org ya 2004, sehemu ya tovuti ya Delray Beach Sister Cities' programme, ilivyohifadhiwa kwenye archive.org, kuangaliwa Agosti 2020 Bruce Heilman na Laurean Ndumbaro, "Corruption, Politics and Societal Values in Tanzania: An Evaluation of the Mkapa Administration's Anti-Corruption Efforts", Afr. J. polit. sd. (2002), Toleo 1 Nambari 7 "Mheshimiwa Benjamin William Mkapa", Bodi ya Wadhamini, Chuo cha AKU, ilitolewa 19-10-2009 Gideoni Burrows, "We sell arms to Saddam's friends", New Statesman, 8 Septemba 2003 Mkapa lauds Kenya's democratic posture. panapress.com (12 October 2005). Iliwekwa mnamo 26 Septemba 2013. 83RD Annual District Conference & Assembly (PDF) (Kiingereza). Page 10, Rotary International District 9200 (17 May 2008). Iliwekwa mnamo 26 Septemba 2013. Prominent Alumni (Kiingereza). Kenyatta University. Iliwekwa mnamo 26 Septemba 2013. Citation: Benjamin William Mkapa DCL (PDF) (Kiingereza). Newcastle University (2007). Iliwekwa mnamo 26 Septemba 2013. UCC honours former Tanzanian leader (Kiingereza). Iliwekwa mnamo 26 Septemba 2013.

H.E. Benjamin Mkapa receives Makerere Honorary PhD (Kiingereza). Makerere University (27 November 2009). Iliwekwa mnamo 26 Septemba 2013.

Viungo vya nje Wikiquote-logo.svg Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu: Benjamin Mkapa

2001 mahojiano na Public Broadcasting Station "Serikali ya Uingereza yagawanyika juu ya mfumo wa radar wa Tanzania" "Blair ashtumiwa juu ya mpango wa rada wa Tanzania" "Mpango wa rada wa Tanzania "upotezaji wa fedha" "Umiliki wa mradi wa nguvu ya makaa ya mawe ya Kiwira : Uhusiano wa Mkapa-Yona" "Rais mstaafu Benjamin Mkapa Kutunukiwa Nishani ya Heshima kwa Kuanzisha Vyuo Vikuu Binafsi Nchini Wakati wa Utawala Wake.1661870/ Benjamin Mkapa bio katika Tume ya Afrika

tanzania.go.tz