Uko hapa: NyumbaniNchiPeopleMkuu wa NchiBiden Joe

Watu Maarufu Tanzania

Mkuu wa Nchi

Biden Joe

Rais wa Marekani

Biden Front
Tarehe ya Kuzaliwa:
1942-11-02
Mahali pa Kuzaliwa:
Marekani

Joe Biden, ni Rais wa 46 wa Marekani, kutoka katika chama cha Democrat aliyehudumu kama Makamu wa 47 wa Rais nchini humo kipindi cha uongozi wa Rais Barack Obama mwaka 2009 hadi 2017.

Amezaliwa tarehe 2, Novemba mwaka 1942, katika mjia wa Scranton uliopo jimbo la Pennsylvania nchini Marekani.

Amesoma katika chuo kikuu cha Delawware kabla ya kujiunga na chuo kikuu cha Syracuse alipopata shahada yake Sheria mwaka 1968.

SAFARI SIASA ZA BIDEN Mstari wa siasa za Biden ulichorwa kwa mara ya kwanza alipochaguliwa kuwa seneta na baraza la mji wa New Caste mwaka 1970 na kuingia katika historia ya kuwa kijana mdogo kushika nafasi hiyo.

Akiwa na umri wa miaka 29 aliteuliwa tena kuwa Seneta katika jimbo la Delawere, kazi aliyoifanya kwa weledi mkubwa sana kiasi cha kumfanya ajulikane zaidi na sifa zake kusambaa.

Akiwa Seneta, Biden alijiimarisha kuwa mwanasiasa wa karibu, mpatanishi na mwenye uwezo wa kufikia makubaliano na wapinzani wake.

Aliteuliwa kuwa Seneta mwenye kushughulikia kampeni za Rais , akatwaa nafasi nyingine ya kuwa Seneti katika kitengo cha Mahakama aliposghulikia masuala ya haki, kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya.

Ameshika wadhifa wa kuwa Senate wa masuala ya Mambo ya Nje kwa miaka 12, akiwa anashughulikia kwa ukaribu masuala ya kuwezesha miradi ya nje ya nchi inayofanywa na taifa lake.

Ni katika kipindi hicho , ambapo alifanya maamuzi ambayo hayakupongezwa sana, kama sheria ya haki ya jinai ya 1994 aliandika na kupitisha wakati wa utawala wa kwanza wa Bill Clinton.

Marekebisho hayo yalilenga kupunguza machafuko yaliyozidi miongo kadhaa, lakini ilisababisha kufungwa kwa watu wengi, na athari kubwa kwa watu weusi na Walatino.

Kwa kazi yake ya muda mrefu ya seneta, lazima tuongeze miaka yake nane akiwa Makamu wa Rais wa Obama (2009-2017), ambaye alijenga uhusiano mzuri zaidi.

Urafiki kati ya Obama na Biden ulinaswa katika picha nyingi za utawala wake na wakati uliofuata Akiwa Makamu wa Rais, chini ya utawala wa Rais Barack, aliweza kuhakikisha sheria ya kupunguza Matumizi iliyojulikana kama "Budget Contol Act 2011" inapitishwa ili kuliokoa taifa hilo kutopata mporomoko wa uchumi, pia anakumbukwa kwa kuwezesha sheria ya Kulipa kodi iliyojulika kwa "Americans Taxpayer relief" ya mwaka 2012.

Weledi na ustadi wake katika kutimiza majukumu kulimfanya Rais Obama ampe medali ya heshima ya "Presidential Medal Freedom" ikiwa ni mwaka 2017.

Biden alitupa karata zake kuwania nafasi ya urais nchini humo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 akiwa ameambatana na mwanamama mashuhuri na nguli katika siasa Kamala Hariss,wakichuana vikali na aliyekuwa rais wa nchiyo kwa wakati ule, Donald Trump.

uchaguzi huu umetajwa kuwa moja kati ya chaguzi zilizotoa cheche sana kutoka na machahari kutok pande zote mbili.

Biden alifanikiwa kushinda uchaguzi huo huku wakiweka historia mpya kwa kuwa Rais mwenye umri mkubwa pia kuwa na makamu mwanamke.

Mapema mwezi Januari tarehe 20, aliapishwa rasmi kuwa Rais wa nchi hiyo. Siku mia za kwanza za utumishi wake kama Rais wa nchi hiyo, aliweza kusaini mikatabata 17 mapema ndani ya siku mbili za kwanza na kuweka rekodi mpya kwani haikuwahi kutokea katika historia ya nchi hiyo.

Utawala wake unatajwa kuwa utawala uliojaa demokrasia, wengi wakimsifu kwa uwezo wake mkubwa wa kutatua migogoro hasa inayoihusisha taifa lake.

Mapambano dhidi ya ugonjwa wa COVID-19, upatikanaji wa chanjo ya ugonjwa huo, kuondoa vikosi vya kijeshi nchini Afganistan vilivyodumu takribani miaka 20 katika taifa hilo,

Huwezi kuzungumzia sifa za biden pasipo kutaja tukio la Mexico, mara baada ya kupitisha sheria ya mabadiliko inayo waruhusu wahamiaji kutoka nchini humo kupata makazi katika taifa lao ikiwa ni pamoja na ulinzi pasipo kuyakimbia makazi yao.

Vita kati israel na Pakistan iliyoinuka mapema mwezi Mei, Rais Biden alionesha msimamo wa taifa hilo kuwa lipo tayari kuisaidia Israel.

MAISHA YA BIDEN KATIKA FAMILIA, MAUMIVU NA NDOA Usichokijua katika maisha ya Rais huyu ni kuwa aliwahi kuoa na kufanikiwa kupata watoto watatu, wakiume wawili na mmoja wa kike. Mke wake alikuwa akiitwa Neilia, na mtoto wake wa kwanza wa kiume aliitwa Beau wa pili aliitwa Hunter na watatu aliitwa Naomi.

Alimpoteza mke na mtoto wake wa kike katika ajali ya gari mwaka 1972 zikiwa zimepita wiki mbili tangu ateuliwa kuwa seneta wa Delaware.

Ambapo kabla ya kifo cha mke wake na mtoto, walililazwa katika moja ya hospitalikubwa mjini hapo.

MAUMIVU kupoteza mke na mtoto kulivuruga mipango yote aliyokuwa amejiwekea katika kipindi hicho inaelezwa kuwa Biden alifikiria kuachia madaraka hayo maamuzi yaliyopingwa vikali na baraza la masenate katika mji wa Delaware.

ilimchukua muda kuweza kukubaliana na ukweli kuwa hawapo tena na maisha yake yanapaswa kusonga hususiana adhma yake ya kuongoza wananchi wa eneo hilo.

NDOA alikutana mke wake wa pili mwaka 1975, mwanamama Jilly Trace Jacob, ambaye kitaaluma ni mwalimu, walifunga ndoa mwaka 1977 na kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike Ashley Biden.

TanzaniaWeb