Uko hapa: NyumbaniNchiPeopleBurudaniFatuma Baraka

Watu Maarufu Tanzania

Burudani

Fatuma Baraka

Mfahamu Bi. KIdude

Kiduude
Tarehe ya Kuzaliwa:
N/A
Mahali pa Kuzaliwa:
Unguja
Date of Death:
2013-04-17
DECEASED

Fatuma Binti Baraka anaefahamika kama Bi Kidude, anakisiwa kwamba amezaliwa 1910, akiwa mtoto wa muuza nazi aliyegeuka kuwa msanii maarufu visiwani Zanzibar na kwengineko kwa ujumla.

Yeyote akimuuliza kuhusu umri wake wake anasema hawezi kuutaja lakini alizaliwa zama za sarafu ya rupia. Ilikuwa sarafu iliyotumiwa katika eneo la Afrika Mashariki mpaka wakati wa vita vya kwanza vya dunia. Bi Kidude si kwamba alikuwa na mvuto kwa sauti yake nzuri ya kuimba taarab lakini pia namna ya muonekano wake katika jukwaa. Ingawa alikuwa mzee lakini alikuwa maarufu na mwenye kufurahisha watu wa umri tofauti hadi vijana.

1920, Bi Kidude alikuwa akiimba rasmi katika matamasha ya kitamadauni. Alizaliwa katika kijiji kidoko Mfagimalingo mjini Unguja, alikuwa ni mwimbaji wa kwanza wa kike katika eneo la Zanzibar. Ilikuwa ni hatua kubwa kwa wanawake hasa wanawake wanaovaa baibui vazi la kujisitiri kwa wanawake wa Pwani ya afrika mashariki.

Alikuwa na ujasiri mkubwa wakati alipotoroka katika visiwa vya Zanzibar kukwepa ndoa ya lazima akiwa na umri wa miaka 13. Baadae akawa mtu anaejihusisha sana na muziki wa taarab kwa kufanya ziara mbalimbali za muziki huo katika maeneo ya afrika mashariki.

Baada ya kurejea Zanzibar 1940, pamoja na kuwa mtu mwenye umaarufu mkubwa lakini aliendelea kuishi katika nyumba yake iliyotengenezwa kwa udongo. Mbali na muziki alikuwa akijihusisha na vyama vya kijamii na kutoa elimu ya unyago kwa wasichana katika visiwa hivyo.

Kwa kutumia muziki wenye hisia na huzuni Bi Kidude aliimba kwa mtindo wa aina yake wenye mvuto. Hakuweza kujali kuhusu miiko, aliolewa mara mbili, na alikuwa anavuta sigara na mwaka uliyopita akikuwa anakunywa sana pombe. Katika jamii isiyopenda mabadikilo lakini aliweza kuishi.

Wakati akiwa katika jukwaa alikuwa akipenda kubadili miondoko. Kwa hiyo alikuwa akitoa wakati mgumu sana kwa wanamuziki wanaompogia vyombo mbalimbali katika bendi husika kwa wakati huo.

Washabiki wake walikuwa wakipenda sana mawazo yake ya kubadili miondoko au nyimbo akiwa katika jukwaa. Ingawa mwanamke huyo alikuwa mwenye umbo dogo lakini alikuwa akipiga ngoma katika kiwango cha kushangaza.

Mirindimo yake na namna alivyokuwa na nguvu na uwezo wa kupiga ngoma ilikuwa ikishangaza sana idadi kubwa ya watu mpaka mwaka uliyopita. 2005 alipata tuzo kutokana na kutukuza muziki na utamaduni wa Zanzibar. Bi Kidude alifariki mwaka 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu katika nyumba yake ndogo mjini Zanzibar ambayo ndimo yalikuwa makazi yake.Alizikwa na maelfu ya watu, Wakazi wa visiwa vya Zanzibar na kwengineno wanaomboleza kifo cha malkia wa Taarab Bi. Kidude.

Mitandao