Uko hapa: NyumbaniNchiPeopleBurudaniFaustina Charles Mtinanga

Watu Maarufu Tanzania

Burudani

Faustina Charles Mtinanga

Historia ya Nandy

Nandigooo
Tarehe ya Kuzaliwa:
1992-11-23
Mahali pa Kuzaliwa:
Moshi

Msanii maarufu nchini Faustina Charles Mtinanga anayetambulika kama Nandy , akianza afari yake ya elimu katika shule ya msingi Mawenzi na baadae kujiunga shuke ya sekondari Lomwe , alipomaliza alifanikiwa kujiunga na chuo cha Biashara CBE , Dar es salaam.

Alianza kupenda mziki tangu akiwa mdogo alipokuwa na umri wa miaka mi tano alikuwa mwanachama hai wa kwaya ya mafunzo katika kanisa la KKT huko moshi. na alipokuwa akisoma shule ya Sekondari Lomwe alijiunga na kikundi cha kwaya na alifanikiwa kuwa mwanakwaya mkuu katika shule hiyo.

Kazi yake ilianza kujulikana baada ya rafiki yake kumtambulisha kwa Marehemu Ruge Mutahaba aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania House of Talent (THT). Hapa ndipo alipokutana na Ema the Boy, ambaye ndiye aliyekuja kumtayarishia kibao chake maarufu cha Nagusagusa.Wimbo ulikuja kutamba mno wiki tu tangu kutolewa kwake.

Mwanzoni mwa mwaka wa 2016 alishiriki kwenye mashindano ya kuimba yaliyoandaliwa na Tecno. Shindano lilishirikisha washiriki wengine kutoka nchi kibao za Afrika na kipindi cha fainali kilichofanyika huko Lagos, Nigeria, Nandy aliibuka kama mshindi wa pili. Shindano hili lilimkuza kimuziki, hasa katika suala zima la utumbuizaji jukwaani, alipata maarifa ya muhimu kutoka kwa magwiji wa muziki kama vile akina M.I Abaga, Yemi Alade na Bien wa Sauti Sol.

Mwaka wa 2017 alitoa kibao cha One Day ambacho kilisukuma kazi yake na hatimaye kumpa nafasi kadhaa zilizomfanya kushiriki kwenye Coke Studio Africa 2017 na mwaka huohuo akaja kuchaguliwa kwenye tuzo za All Africa Music Awards katika kundi la wanamuziki bora wa kike kutoka Afrika Mashariki na kuibuka mshindi.

Maendelo ya Nandy katika mziki yameidi kukuua siku hadi siku na pia amefanikiwa kufanya Colabo na wasanii mbalimbmbali ikiwe kundi la wasanii kutoka Kenya Saut soul walitoa nyimbo itwayo Kiza Kinne na ilifanikiwa kupokelewa vizuri na mashabiki

Mnamo mwaka 2019 nandy alishinda Tuzo ya BEST FEMALE African Entertainment Awards USA 2019(AEAUSA)na kuliletea Taifa heshima kwa kuonesha jitihada ya kazi anazofanya na zinavyokubalika Dunian Hata hivyo mwaka 2020 alifanikiwa kushinda Tuzo ya AFRIMMA BEST FEMALE EAST AFRICA.

Mwaka 2021 , Nandy amefanikia kufanya Colabo na wasanii wawili wa njee . alianza kufanya na msanii JoeBoy kutoka Nigeria wakatoa nyimbo itwayo Number One . Baada ya miezi kadha alifanikiwa kufanya Colabo na Msanii Mkongwe Koffie Lomide anaye ishi nchini Ufaransa walitoa nyimbo itwayo Leo Leo". Koffie Lomide ni moja ya wasanii wakongwe wanaomkubali sana Nandy.

Kuachilia maswala ya Mziki , July 2020 Nandy aliamua kuwekeza kwenye biashara na kufungua Nandy Bridal iliyopo Mbezi Beach Dar es Salaam, ndani ya Nandy bridal anauza nguo za maharusi pia kunasaluni ya wanawake na sehemu ya kufanyiwa massage. Alisema ameamua kufungua Biashara kwakuwa ni kitu anachopenda kufanya pia.

TanzaniaWeb