Uko hapa: NyumbaniNchiPeopleSiasaFreeman Mbowe

Watu Maarufu Tanzania

Siasa

Freeman Mbowe

Mwenyikiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA

Mbowe11
Tarehe ya Kuzaliwa:
1961-09-14
Mahali pa Kuzaliwa:
Tanzania

Freeman Aikael Mbowe alizaliwa tarehe 14/09/1961 Wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro, ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kwa Miaka 17 mfululizo.

Pia miongoni mwa Watu waliofanya Kazi katika Bank kuu ya Tanzania kama Afisa wa Bank Kuu (BoT) akiwa chini ya Edwin Mtei, Bob Makani. SIASA

Katika harakati za kisiasa, Freeman Aikael Mbowe aliingia rasmi katika siasa mwaka 1992. Akiwa ni miongoni mwa WAASISI au waanzilishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) chama ambacho kilisajiliwa usajili wa kudumu mwaka 1993 kwa namba 0000003 kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992 .

Mbowe akiwa ndio kijana mdogo kuliko Wote wakati wa uasisi wa CHADEMA aliingoza kurugenzi ya Vijana ya CHADEMA chini ya Uenyekiti wa Edwin Mtei. Busara, Hekima na utulivu wake katika kutatua na kufanya maamuzi kulimpa nafasi kubwa sana ndani ya chama hicho.

Alifanikiwa kuwashawishi viongozi wake wa Chama hicho kwa wakati huo akiwa ni Edwin Mtei na Bob Makani kuwa waungane na Chama cha NCCR MAGEUZI kusimamisha mgombea mmoja kwa kumuunga mkono Mgombea Augstine Lyatonga Mrema, ushauri uliopokelewa kwa mikono miwili.

Mbowe alichukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la Hai mwaka 1995. wakati wa Kampeni jimbo la Hai , aliombwa kugharamia Mkutano wa mgombea urais Lyatonga Mrema na aliahidiwa kwamba Mrema atamnadi jukwaani. kwa kuwa alikua na Fedha na uchumi mzuri, aligharamia Mkutano na malazi ya timu ya kampeni ya Mrema.

Lakini Mrema alipofika Jukwaani alimpuuza Freeman Mbowe wa CHADEMA na kumnadi mgombea wa NCCR MAGEUZI aliyeitwa Mwinyihamisi Mushi. Katika uchaguzi huo Mgombea wa NCCR MAGEUZI Mwanahamisi Mushi alishinda kwa kupata kura 29,046 (52.0%) huku Freeman Mbowe akiambulia kura 15,995 sawa na asilimia 26 tu. Hakukata tamaa, Mwaka 2000, aligombea tena ubunge jimbo la Hai na kupata ushindi mnono wa kura 64.5% dhidi ya mpinzani wake wa NCCR MAGEUZI ambaye alipata mweleka kutokana na chama chake kuwa na mvurugiko.

Mwaka 2004, aligombea uenyekiti wa CHADEMA TAIFA na kushinda akimpokea Bob Makani ambaye aliongoza kuanzia mwaka 1999, baada ya kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA alifanya mabadiliko makubwa Sana ndani ya chama.

Huwezi kuwataja vinara wa Upinzani kwa sasa nchini bila kuwataja vijana kwa wakati ule walionolewa na Mbowe, alifanikiwa kumuibua John Mnyika, Zitto Kabwe, Halma Mdee, Tundu Lissu.

Mwaka 2005, aligombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa na mgombea mwenza kutoka Zanzibar bwana Jumbe Rajab Jumbe ambaye alifariki siku chache kabla ya uchaguzi mkuu uliokua ufanyike tarehe 30/10/2005 na hivyo uchaguzi kuahirishwa mpaka tarehe 14 /12/2005.

Chama kilifanya tena uchaguzi wa ndani, na aliteuliwa tena kuongoza chama hicho, na katika uchaguzi wa urais mwaka 2010 alianzisha kampeni iliyoitwa MOVEMENT FOR CHANGE.

Katika uchaguzi Mkuu mwaka 2015,Freeman Mbowe aligombea ubunge jimbo la Hai na kushinda kata zote 16 kasoro moja ya 17 ambayo uchaguzi uliahirishwa baada ya mgombea kufariki. Mbowe alishinda uchaguzi kwa kupata kura 51,124 huku mgombea wa CCM Dastan Mally akipata kura 26,996,Nuru Muhammed wa ACT Wazalendo akijizolea kura 315 na Ndashuka Issa wa APPT - Maendeleo akijinyakulia kura 279.

Katika nafasi ya Urais, Mbowe na kamati kuu walishirikiana kumuingiza Edward Lowassa ndani ya CHADEMA na kupeleka Jina Lake Baraza kuu na hatimaye kupitishwa na Mkutano mkuu wa CHADEMA tarahe 04/08/2015 kama mgombea urais wa CHADEMA anayeungwa mkono na UKAWA.

Baada ya uchaguzi Mkuu 2015 , Freeman Aikael Mbowe aliunda Serikali mbadala (Shadow Government) au Kambi rasimi ya Upinzani Bungeni (KUB/KRUB) mapema mwaka 2016 ambayo inahusisha vyama vyote ndani ya UKAWA.

CHADEMA, bado ina imani na uongozi wa Mbowe, kwa kulithibitisha hili, wamempa tena wadhifa wa kuongoza chama hicho katika uchaguzi uliofanyika mwaka 2019.

CHANGAMOTO ZA SIASA

Katika safari ya kukiongoza chama cha CHADEMA, Kiongozi huyu amepita katika nyakati tofauti.Lakini kinachoonekana juu yake ni kutokata tamaa na kuwa na Imani kubwa juu kile anacho kilenga.

Mwaka 2018, Mbowe amewahi kushtakiwa pamoja viongozi wengine ndani ya Chama chake kwa makosa ya Kuharibu uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Kinondoni, pia kusababisha mauaji ya Mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji, Akwilina Akwilini, aliyeuwawa wakati wa vurugu za wanachama wa chama hicho na Polisi.

Kesi hii ilichukua takribani miaka miwili kumaliza, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliwakuta na Hatia, ya Makosa 12 kati ya 13 walioshitakiwa nayo mwaka 2018.

Mahakama iliamuru kuwa walipe faini ya shilingi milioni 350 ama watumikie kifungo cha miezi 5 Jela.

walifanikiwa kulipa faini hizo, chini ya nguvu ya umma, na kuweza kuachiwa huru. Mwaka 2020, katika kampeni za ubunge jimbo la Hai, kiongozi huyo alipokea vitisho vingi kutoka kwa moja wa Polisi aliyesisika akisema kuwa kiongozi huyo ata afanye nini hatoweza kushinda tena nafasi. mwisho wa uchaguzi huo alishindwa dhidi ya mgombea wa CCM, Saasisha Mafuwe. Mara bada ya Uchaguzi kuisha, CHADEMA iliendeleza Kampeni ya Katiba, na safari hii,mambo hayakwenda kama hapo miaka ya nyuma.

Akiwa jijini Mwanza, kwa ajili ya kuhudhuria Jukwaa la katiba mpya lililoandaliwa na Vijana wa Chama hicho, Mbowe aliingia hatiani na kukamatwa na Jshi la Polisi.

Mbowe alifikishwa Mahakaman ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu tuhuma za Ugaidi alizosomewa .

Usaliti, ni moja ya changamoto ambazo kiongozi huyu amezipitia kwa ukubwa, Mwaka 2015 Wilbrod Peter Slaa, alikihama Chama hicho na kutimkia CCM, akiwa na hoja nzito ya kutokubaliana na uongozi wa chama hicho wa kumsimamisha Edward Lowassa kama mgombea wa Urais.

Baadae mwaka 2019, Lowassa alihama chama hicho na kurejee CCM, usaliti huu wa kisiasa unatokea Mbowe akiwa ni Mwenyekiti wa chama hicho. viongozi wengi wa CHADEMA walihama chama hicho kwa kasi, na ndipo likaibuka neno "Kuunga Juhudi".

Pigo lingine ni kuteuliwa kwa viongozi 19 wa Chama hicho kinyume cha taratibu za chama, kuwa sehemu ya Bunge wakati chama hicho kikiwa na ajenda kali ya kususia nafasi hizo maalumu za uwakilishi kwa wanawake Bungeni, likaibuka jina la COVID-19, hili bado ni fumbo.

Mbowe amepoteza mali nyingi, bila shaka unaifahamu Bilcanas, ilivunjwa mwaka 2016 , siasa inatajwa kuwa miongoni mwa sababu ya jengo hili kuvunjwa.

TanzaniaWeb