Uko hapa: NyumbaniNchiPeopleSiasaHaikainde Hichilema

Watu Maarufu Tanzania

Siasa

Haikainde Hichilema

Rais Wa Zambia

HHH
Tarehe ya Kuzaliwa:
1962-06-04
Mahali pa Kuzaliwa:
Zambia

Hakainde Hichilema, mfanyabiashara aliyejitengenezea utajiri wake, ni kiongozi kijana wa chama kikuu cha upinzani nchini Zambia kijulikanacho kama United Party for National Development (UPND).

Alizaliwa Juni 4, 1962 kusini mwa Monze, na kuanzasafari yake ya masomo katika eneo hilo alilozaliwa na kufanikiwa kujiunga na chuo kikuu cha Zambia kwa ufradhili wa Serikali, aliposoma na kuhitimu shahada ya sanaa katika uchumi na biashara mnamo mwaka 1986.

Baadaye alipata shahada ya uzamili ya somo la Fedha na Biashara (MBA) kutoka Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingereza.

Alijulikana kwa upendo na wengi hupenda kumuita kwa utani jina la HH, ameandika rekodi ya kuvutia katika biashara, ndani na nje yamipaka ya Zambia.

Anatajwa kuwa mFugaji mahiri zaidi nchinu humo,huku akishika nafasi ya pili kwa ufugaji nchi nzima kwa kuwa na zaidi ya mifugo 100,000. hivyo kupelekea kuwa msambazaji mkubwa wa nyama katika soko la ndani l nchini humo.

Sio hapo tu, uwekezaji wake umepiga tambo zaidi hadi sekta ya utalii, inaelezwa kuwa amewekeza katika sekta hii ambayo ndiyo kitovu mama cha uchumi katika mataifa mengi barani Afrika.

Kufuatia elimu yake ya chuo kikuu, Hichilema alipanda katika nafasi za juu katika ulimwengu wa mashirika nchini Zambia, akipata kazi za kifahari kama Mkurugenzi wa kampuni ya Coopers na Lybrand akiwa na umri wa miaka 32, kutoka 1994 hadi 1998, na baadaye kama mrithi wa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Cooper, Grant Thornton, kutoka 1998 hadi 2006.

Alikuwa pia mkubwa zaidi katika kampuni mbili zinazomilikiwa na wageni ikiwa ni pamoja na Benki ya Barclays Zambia.

Aidha, Hichilema ni mtaalamu wa majadiliano ya Biashara, na ni mwanachama wa Taasisi ya Wakurugenzi ya Zambia.

Bwana HH ,alishinda urais wa chama cha upinzani UPND, mnamo mwaka 2006 kufuatia kifo cha kiongozi wake, Anderson Mazoka, mshauri wake wa biashara ambaye pia alikuwa rafiki yake wa karibu.

Tangu wakati huo wanasiasa wa chama tawala, bila mafanikio, walikuwa wakijaribu kumuhusisha na kesi za kisheria ambazo amekataa kuziacha ziwe kuzuizi cha kufikia ndoto zake.

Katika uchaguzi mdogo wa urais wa Januari 2015, Hichilema alikuwa wa pili katika kinyanganyiro hicho nyuma ya mgombea wa chama cha PF aliyekuwa madarakani, akipungukiwa na kura 27,000 tu.

Ameendesha kampeni zake akiegemea zaidi suala la uchumi, akisema kwamba Zambia inahitaji kiongozi anayeelewa biashara na anayeweza kugeuza uchumi ili kufungua faida za maendeleo katika afya, elimu na nyanja zinginezo.

Ana shauku ya kuboresho mfumo wa elimu wa Zambia ili kila Mzambia mchanga apate fursa aliyopata ya kupokea msaada wa serikali ambao unaweza kuwawezesha vijana kuanzisha taaluma nzuri na kuwawezesha kupata mshahara mzuri, kukidhi mahitaji ya familia zao na kusaidia katika ukuaji wa uchumi wa Zambia.

Na pia, Hichilema sio mwanasiasa tu na mfanyabiashara pekee, pia ni mfadhili, akichangia pakubwa shughuli za jamii na miradi kama kliniki, shule, ujenzi wa visima na kujenga mabwawa ili kuboresha shughuli za kilimo.

Amefunga pingu za maisha na Mutinta na kwa pamoja wamejaaliwa watoto watatu.

TanzaniaWeb