Uko hapa: NyumbaniNchiPeopleSiasaJanuary Makamba

Watu Maarufu Tanzania

Siasa

January Makamba

Waziri wa Nishati

January1
Tarehe ya Kuzaliwa:
1974-01-28
Mahali pa Kuzaliwa:
Tanzania

January Yusuph Makamba, amezaliwa mwaka 1974 tarehe 28 mwezi januari, katika mkoa wa Siginda akiwa ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto wanne.

Ni mwanasiasa nguli nchini Tanzania katika Chama tawala cha Mapinduzi CCM, amekuwa na kulelewa katika misingi ya siasa za CCM, baba yake amekuwa Katibu Mkuu katika chama hicho. ELIMU na KAZI Amesoma katika shule ya msingi Handeni , na sekondayi amesoma katika shule ya Galanos, kisha elimu ya kidato cha tano ameipata katika shule ya Forest Hill ya Morogoro.

Amesoma katika chuo cha Quincy College kilichopo Marekani, kabla ya kwenda kuchukua Shahada ya Uzamili ya masuala ya usuluhishi katika chuo cha George Mason mwaka 2004.

Alipohitimu elimu yake alirejeea nyumbani na kuanza kufanya kazi katika Wizara ya Mambo ya nje kama ofisa utumishi wa mambo ya nje wakati huo msatafu Jakaya Kikwete akiwa ndiye Waziri katika Wizara hiyo. Mwaka 2005 alikuwa nmstari wa mbele katika kumpigia kampeni Kikwete katika uchaguzi Mkuu wa urais, aliyeibuka na ushindi wa asilimia 80.

Alichaguliwa kuwa msaidizi binafsi wa rais, nafasi aliyoitumikia kwa miaka mitano. SIASA Mwaka 2010 aligombea nafasi ya Ubunge katika uchaguzi Mkuu jimbo la nyumbani kwao Bumbuli, alipita bila kupingwa, amehudumu toka 2010 hadi sasa. Amekuwa pia mjumbe wa kamati ya Nishati na Madini ya Bunge la kumi. Mwaka 2011 alichukua nafasi ya Bernad Membe ndani ya CCM akawa Katibu wa masuala ya Siasa na uhusiano wa Mataifa, alihudumu hadi mwaka 2012.

Alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya Taifa NEC. Mwaka 2012 aliteuliwa tena kuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia. Januari ni mwepesi katika masuala ya jamii, mwaka 2014 alikubali wito aliotumiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, wa kushiriki katika tamasha la kueilimisha jamii juu ya ugonjwa wa Fistula ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wagonjwa wa Fistula, aliweza kuchangia kiasi cha Milioni Moja kuwasaidia wagonjwa hao.

Mwaka 2015 alitangaza nia ya kugombea urais, lakini suala hili alianza kuliongelea tangu mwaka 2014 na anatajwa kuwa mgombea wa kwanza kutangaza nia yake ya kugombea. Katika Kampeni za Urais wa mwaka 2015, Makamba alizindua kitabu kilichoandikwa na Fr. Karugendo, kilichokuwa na maswali 40 aliyoulizwa , jina la kitabu lilikuwa ni "Mazungumzo na Januari Makamba. Mchakato wa kura za maoni wa CCM ulimteua Hayati Magufuli kuwa mgombea atakaye gombea nafasi ya Urais, na hapo Makamba ilimpasa kurejea Jimboni mwake alipochukua fomu tena kutetea kiti chake cha uwakilishi.

Aliteuliwa kuwa Waziri wa Muungano na Mazingira mwakanafasi aliyohudumu hadi mwaka 2020. Akiwa Waziri alifanikiwa kutokomeza matumizi yamifiku ya olastiki nchini kote. Kwasasa kiongozi huyu ni Mbunge katika jimbo hili hilo la Bumbuli, na anatajwa kuwa kiongizi mwenye weledi mkubwa katika kutatua masuala mbali mbali.

Tarehe 12, septemba 2021, katika uongozi wa awamu ya sits chini ya Rais Samia, Makamba anarejea tena katika Baraza la Mawaziri kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Nishati akichukua nafasi ya Dr. Medard Kelemani.

TanzaniaWeb