Uko hapa: NyumbaniNchiPeopleTraditional RulersJenerali Venance Salvatory Mabeyo

Watu Maarufu Tanzania

Traditional Rulers

Jenerali Venance Salvatory Mabeyo

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania

GEN MABEYO
Tarehe ya Kuzaliwa:
N/A
Mahali pa Kuzaliwa:
Tanzania

enerali Venance Mabeyo ni Mkuu wa Majeshi wa nane kuliongoza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tangu alipoteuliwa tarehe 06 February 2017 na Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya tano, Dk. John Pombe Magufuli.

Jenerali Venance Mabeyo alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tarehe 01 January 1979 na kuhudhuria kozi ya afisa mwanafunzi na kupata kamisheni mwaka 1980 kuwa Luteni Usu.

Jenerali Venance Mabeyo alihudhuria kozi mbalimbali ndani na nje ya nchi, baadhi ya nchi hizo ni Kenya, India, Canada na Marekani Jenerali Venance Mabeyo katika kulitumikia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania alishika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Mwambata Jeshi nchini Rwanda, Msaidizi wa Mkuu wa Majeshi , Mkuu wa Tawi la Usalama na Utambuzi na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ.

Jenerali Venance Mabeyo ametunukiwa medali mbalimbali

• Miaka 20 ya JWTZ • Medali ya utumishi mrefu. • Medali ya miaka 40 ya JWTZ. • Medali ya utumishi uliotukuka. • Medali ya Comoro na Anjouan. • Medali ya miaka 50 ya uhuru • Medali ya miaka 50 ya muungano pamoja na • Miaka 50 ya JWTZ.

Taarifa za Serikali