Uko hapa: NyumbaniNchiPeopleSiasaJuma Aweso

Watu Maarufu Tanzania

Siasa

Juma Aweso

Waziri wa Maji na Umwagiliaji

Juma Awesoww
Tarehe ya Kuzaliwa:
1985-03-22
Mahali pa Kuzaliwa:
Tanzania

Juma Hamidu Aweso ndio majina aliyopewa na wazazi wake, kiongozi mdogo wa siasa nchini Tanzania. Amezaliwa mwaka 1985 tarehe 22 ya mwezi March. Jumaa Hamidu Aweso alizaliwa tarehe 22 Machi 1985, Pangani, Mkoani Tanga. Aweso amesoma katika Shule ya Msingi ya Mwambao, Pangani, Mkoani Tanga 1994-2000 na Elimu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari Bagamoyo 2001 hadi mwaka 2004. Aweso alipata Elimu ya Juu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari ya Pugu 2005 hadi mwaka 2007. Kati ya mwaka 2007 na 2009, Aweso alihudhuria Chuo cha Ualimu cha Morogoro na kutunukiwa Astashahada ya Ualimu. Juma Aweso ana Shahada ya Sayansi katika Kemia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, aliyotunukiwa mwaka 2013. Mwaka 2018 hadi 2020 Aweso alihudhuria na kuhitimu Shahada ya Pili ya Utawala na Uongozi Governance and Leadership ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT). Alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Pangani lililopo Mkoani Tanga mwaka 2015. Mwezi Oktoba 2017, Mhe. Aweso aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, akichukua nafasi ya Mhe. Kamwelwe aliyeteuliwa kuwa Waziri. Oktoba 2020, alipita bila kupingwa kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Mbunge wa Pangani kwa Awamu ya Pili, kwa mwaka 2020 hadi 2025. Mwezi Desemba 2020, aliteuliwa kuwa Waziri wa Maji. Hivi sasa ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji katika serikali ya awamu ya sita iliyo chini ya uongozi wa Rais Samia. ELIMU Historia ya elimu ya kiongozi huyu ilianza mwaka 1994 katika shule ya msingi ya Mwambao, kisha akasoma bagamoyo sekondary, na kumalizia katika shule ya sekondari Pugu. Elimu ya juu amesoma katika Chuo Kikuu Dar es Salaam mwaka 2013 alipohitimu Shahada ya Kemia. SIASA Alianza siasa mara tu baada ya kuhitimu elimu yake ya chuo, na kuteuliwa kuwania Ubunge mwaka 2015 na kuibuka kidedea katika uchaguzi huo. Akiwa mwanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM, aliweza kuteuliwa kuwa mwenyekitiwa umoja wa vijana UVCCM katika mkioa wa Tanga, alikuwa ni mmoja kati ya wajumbe wa kamati ya Wilaya, mkoa, Kamati Kuu ya CCM taifa. Katika utawala wa awamu ya tano chini ya uongozi wa Hayati Magufuli, aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji akiwa chini ya Waziri Makame Mbarawa, na mnamo mwaka 2020 aliteuliwa tena kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji. Hivi sasa Wabunge wenzie wamempa jina la Mpambanaji wa nje, kwa sababu ya utendaji wake mkubwa wa kazi anaoufanya katika wizara hiyo, ni Waziri anaetimiza majukumu yake kwa ukubwa akiwa nje ya Wizara. Katika utawala wa Awamu ya Sita wa Rais Samia, Wizara hii inatenda kazi chini ya sera ya "kumtua mama ndo ya maji" Kwasasa anatekeleza mradi wa maji kwa wa miji 28 Tanzania,ili kuhakikisha kuwa huduma ya maji inamfikia kila mtanzania.

TanzaniaWeb