Uko hapa: NyumbaniNchiPeopleSiasaKassim Majaliwa Kassim

Watu Maarufu Tanzania

Siasa

Kassim Majaliwa Kassim

Waziri Mkuu wa Tanzania

Kassim Majaliwa
Tarehe ya Kuzaliwa:
1960-12-22
Mahali pa Kuzaliwa:
Tanzania

Kassim Majaliwa (* 22 Disemba 1960) ni mwanasiasa nchini Tanzania. Alikuwa mbunge wa jimbo la Ruangwa tangu mwaka 2010 akigombea kwa CCM.

Tarehe 19 Novemba 2015 aliteuliwa na rais John Magufuli kuwa waziri mkuu wa serikali ya awamu ya tano nchini Tanzania.

Aliwahi kushika vyeo vya naibu waziri wa utawala wa mikoa na serikali ya mitaa katika ofisi ya waziri mkuu tangu mwaka 2010 na mkuu wa mkoa wa Lindi kuanzia 2006 hadi 2010.

Majaliwa ni mwenyeji wa Mnacho katika Wilaya ya Ruangwa aliposoma shule ya msingi kati ya 1970 hadi 1976. Akaendelea kusoma kwenye Shule ya Sekondari Kigonsera hadi 1980. 1984-1986 alifanya kazi ya ualimu huko Lindi na tangu 1988 aliajiriwa na wizara ya elimu.

1991 akajiunga na chuo cha ualimu Mtwara akaendelea na masomo ya digrii ya kwanza kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, tangu 1999 masomo ya digrii ya pili kwenye Chuo kikuu chs Stockholm (Uswidi) aliyomaliza 1999. Mwaka 2000 alipewa kazi ya Mkuu wa Wilaya.

Ni mpenzi wa michezo ya soka.

TanzaniaWeb