Uko hapa: NyumbaniNchiPeopleSiasaLiberata Mulamula

Watu Maarufu Tanzania

Siasa

Liberata Mulamula

Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Mula 2 Mula2
Tarehe ya Kuzaliwa:
1956-04-10
Mahali pa Kuzaliwa:
Tanzania

Liberata Mulamula, amezaliwa tarehe 10 mwezi Aprili mwaka 1956, ni mwanadiplomasia na mwanasiasa hapa Tanzania. Hivi sasa ni Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki mara baada ya kuteuliwa na Rais Samia .

KAZI

Anauzoefu wa miaka 35 kwenye taaluma ya diplomasia pamoja na uongozi wa masuala ya nje katika Serikali ya Tanzania, ubalozi katika nchi za Canada, Marekani na hata Umoja wa Mataifa.

Kabla ya kustaafu kazi yake ya Udiplomasia mwaka 2016, alikuwa akihudumu kama Katibu Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa miezi saba yaani toka mwezi Mei 2015 hadi Disemba 2015.

Pia amewahi kuwa Katibu Mtendaji wa kwanza wa Mkutano wa Kimataifa wa Kanda ya Maziwa Makuu (ICGLR) nchini Burundi, kuanzia Mwaka 2016 hadi 2021. Alisimamia Amani, Utulivu na Maendeleo katika nchi 11 katika Kanda ya Maziwa Makuu ya Afrika.

ELIMU

Alianza elimu ya msingi akiwa na umri wa miaka sita, katika shule ya Msingi ya Serikali maarufu kama Kayumba kwa sasa, na kuendelea katika shule ya sekondari ya wasichana ya Tabora na kuhitimu mwaka 1973, kisha alijiunga na shule ya sekondari ya Mzizima.

Mwaka 1977 hadi 1980 Liberata alikuwa akisoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, akichua Shahada ya Sanaa, inayohusika katika Sayansi ya Siasa na Uhusiano wa kimataifa .

Aliendelea kusoma, na wakati huu alikuwa akifanya Shahada ya Uzamili ya Sanaa katika Serikali na Siasa katika chuo kikuu cha St. John 's cha mjini New York. Baadaye Chuo Kikuu hicho kilimpa Stashahada ya Uzamili katika Sheria ya Kimataifa.

SIASA

Mwana diplomasia huyu, hakuingia kwenye siasa hadi alipoteuliwa na Rais Jakaya kikwete kama Katibu Mkuu wa wizara ya Mambo ya Nje mnano mwaka 2015.

Kufuatia kifo cha ghafla cha Hayati Magufuli, aliteuliwa kuwa Waziri mpya wa Mambo ya nje nafasi aliyoanza kuitumikia kuanzia mwezi March 2021 katika Baraza la Mawaziri la sita nchini Tanzania.

TanzaniaWeb