Uko hapa: NyumbaniNchiPeopleTraditional RulersMamady Doumbouya

Watu Maarufu Tanzania

Traditional Rulers

Mamady Doumbouya

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi

MAMADY
Tarehe ya Kuzaliwa:
1980-03-04
Mahali pa Kuzaliwa:
Guinea

Mamady Doumbouya, Kiongozi Mkuu wa Jeshi la nchiniu Guinea, aliyetekeleza mapinduzi ya Rais Alpha Conde, mapema Tarehe 05, mwezi September mwaka 2021.

Alizaliwa mnamo mwaka 1980, tarehe 04 mwezi March Mashariki mwa Mji wa Kankan nchini Guinea.

Doumbouya ndiye Rais wa sasa wa Guinea mara tu baada ya kufanya mapinduzi hayo na kumkamata aliye kuwa rais wa nchi hiyo kwa madai ya kuzorota kwa uchumi ulio endelevu.

UZOEFU WA KIJESHI.

Ana uzoefu wa miaka 15 wa kijeshi ambayo ni pamoja kufanya misheni nchini Afghanistan, Cote d'Ivoire, Djibouti, Jamhuri ya Afrika ya Kati na ulinzi wa watu mashuhuri Israeli, Cyprus , Uingereza na Guinea.

Kanali huyo anasemekana "amekamilisha vyema" mafunzo ya wataalam wa ulinzi wa kiutendaji katika Chuo cha Usalama cha Kimataifa huko Israeli, kozi ya mafunzo ya makamanda wa shule katika Shule ya mafnzo ya kijeshi Senegal, mafunzo ya afisa msimamizi Chuo cha staff College Libreville (EEML) cha Gabon na Chuo cha Vita huko Paris.

Alihudumu kama mwanajeshi wa kigeni yaani 'legionnaire' katika jeshi la Ufaransa hadi 2018 wakati Conde alipomtaka arudi Guinea kuongoza GFS, iliyoanzishwa mwaka huo.

Tangu 2018, kumekuwa na ripoti kadhaa kwenye vyombo vya habari vya Guinea zikitilia shaka sifa za Doumbouya.

Doumbouya alikuwa miongoni mwa maafisa 25 wa Guinea waliolengwa kwa vikwazo vya EU juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu. Ni kufuatia uvumi wa kuzuiliwa kwa watu katika Camp Dubreka magharibi mwa Guinea lakini vikwazo hivyo vilifutwa haraka.

Alikuwa huko Forecariah, magharibi mwa Guinea, ambapo alihudumu chini ya ofisi ya uchunguzi wa eneo (DST) na huduma za ujasusi.

Doumbouya anaripotiwa kuhudhuria Chuo cha Vita huko Paris, Ufaransa.

MAPINDUZI YA KIJESHI

katika nyakati tofauti, washauri wa masuala ya usalama wa nchi wamekuwa walitilia mashaka juu maisha ya Kanali huyu, na hii ni kutokanana utata unaogubika maisha yake. wengi walioneka kuhoji sana ju ya mali anazomiliki huku wakitiliashaka zaidi kwani haziendani na mshahara anaopokea kiongozi huyo.

Chama cha Wahariri na Waandishi wa Habari nchini humo kinachojulikana kama Friaguinee,mwaka 2014 kilidai kuwa Kanali huyo alinyimwa uraia wa nchini Ufaransa kwa kile kinachodaiwa kuwa na tabia zisizo ridhisha alizowahi kuzifanya wakati wa mafunzo yake nchini humo.

Doumbouya alikuwa miongoni mwa maafisa 25 wa Guinea waliowekewa vikwazo vya EU juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu. Ni kufuatia uvumi wa kuzuiliwa kwa watu katika Camp Dubreka Magharibi mwa Guinea lakini vikwazo hivyo vilifutwa haraka.

Kama ni kengele ya hatari kulia basi ili lilia ipasavyo juuu ya mwenendo wa Kanali huyu, hadi kufikia kufanya mapinduzi haya ambyo kwa sasa ni gumzo duniani kote.

Septemba 05, mwaka 2021, aliongoza jeshi la nchini kufanya mapinduzi ya kumuondoa Rais Conde madarakani kwa madai ya kurejesha nchi hiyo katika utawaa wa haki.

Alinukuliwa kiongea katik akituo cha Televisheni mara tu baada ya kutekeleza zoezi hilo, aliposema kuwa;

"Ubinafsishaji wa maisha ya kisiasa umekwisha. Tutaweka mpango wa mpito ulio wazi na unaojumuisha watu wote. Tutaweka mfumo ambao [sasa] haupo,"

"Hali ya kijamii , kisiasa na kiuchumi ya nchi, kutofanya kazi kwa taasisi za jamhuri, udanganyifu wa mfumo wa haki, ukiukaji wa haki za raia, kutokuheshimu kanuni za kidemokrasia, siasa nyingi katika utumishi wa umma, usimamizi mbaya wa kifedha, umasikini na ufisadi umesababisha jeshi la jamhuri kuchukua majukumu yake kwa watu wa Guinea. "

"Lazima tusaidie watu wa Guinea kutoka katika hali hii kwa sababu tunaihitaji. Tunamsihi kila mtu akae katika kambi yao na aendelee na shughuli zao za za kawaida ambazo ni pamoja na kulinda mipaka."

"Lengo letu ni kuhakikisha kuwa watu wa Guinea wana umoja na wanapata faida zote za nchi. Hatujaja kufanya mzaha na serikali. Tutajifunza kutokana na makosa yote ambayo tumefanya na watu wote wa Guinea. "Alisisitiza Doumbouya.

Swali ni je, Mapinduzi ya Kijeshi ndio njia sahihi ya kupata utawala bora? kwanini swali hili? kwa siku za hivi karibuni kumekuwepo na mapinduzi kadha wa kadha kama yale yaliyotokea Mwezi March mwaka 2021 nchini Mali, Niger, na yale ambayo yamekuwa endelevu nchini Burkinafaso.

Watafiti kutoka nchini Marekani, Jonathan Powell na Clayton Thyne walibaini zaidi ya majaribio 200 ya mapinduzi ya kijeshi yamefanyika Barani Afrika tangu mwishoni mwa miaka ya 1950.

TanzaniaWeb