Uko hapa: NyumbaniNchiPeopleWanadiplomasiaMwele Malecela

Watu Maarufu Tanzania

Wanadiplomasia

Mwele Malecela

Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti wa Magonjwa ya Kitropiki yaliyopuuzwa katika Shirika la Afya Ulimwenguni.

Mwele 1
Tarehe ya Kuzaliwa:
1963-03-26
Mahali pa Kuzaliwa:
Tanzania

Mwele Ntuli Malecela alizaliwa tarehe 26 Machi 1963, alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za kiafya Tanzania (NIMRI). Aliwania nafasi ya mgombea wa uraisi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Kuanzia Aprili 2017 Mwele Malecela amekua akifanya kazi na shirika la chakula duniani (WHO) upande wa Africa kama msimamizi wa maswala ya utawala, sera na ushauri wa kidiplomasia.

ELIMU

Baada ya kuhitimu shahada ya kwanza katika masuala ya wanyama katika chuo kikuu cha Dar es Salaam, alijiunga na taasisi ya tafiti za kiafya (NIMRI) mnamo mwaka 1987.

Katika kipindi hicho Mwele alifafanya tafiti za ugonjwa wa homa ya matende katika kituo cha Amani.

Aliendelea na elimu ya juu katika chuo kiitwacho London School of Hygiene and Tropical Medicine ambako alitunukiwa shahada yake ya pili mwaka 1990 na shahada ya uzamivu mwaka 1995.

Aliendelea na tafiti zake katika taasisi ya NIMRI mpaka kufikia mwaka 1998 ambapo alipewa cheo cha mkurugenzi wa tafiti. Mwaka 2000 Mwele alikua kiongozi wa program ya homa ya matende, ambayo imekua ikifanya kazi katika wilaya takribani 53.

SIASA

Malecela alijiunga na chama cha Mapinduzi, CCM mnamo mwaka 1981 alipokua Kilakala. Kwa wakati huo alihitajika kupata mafunzo maalumu kwanza kabla ya kujiunga na chama cha mapinduzi. Dokta Malecela alifanya mafunzo hayo mwezi Aprili 1981 na baada ya hapo amekua mwanachama wa kudumu hadi kufikia sasa.

KAZI

Alijiunga na taasisi hiyo mwaka 1987 baada ya kuhitimu Shahada ya Kwanza ya Sayansi katika stadi ya wanyama na tabia zao (BSc in Zoology) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwaka 1986. Baada ya usahili mzito, alipangiwa kufanya kazi Kituo cha Amani (Amani Centre), hususan kushughulikia ugonjwa unaofahamika kama Bancroftian Filariasis.

Kwa maelezo yake, anasema kuwa alishawahi kuusikia ugonjwa huo kipindi akiwa mwanafunzi katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam, ila hakuwahi kujua kama utauanyia kazi.

Aliwaza sana na kutamani kufanya tafti uu ya ugonjwa wa Malaria, kwa kuwa aliona ni eneo la kuvutia zaidi katika tafti.

Amewahi pia kufanyakazi katika maabara ya minyoo (helminthology laboratory) ambapo alijifunza kuhusu parasaiti aitwaye Wuchereria Bancrofti, ambaye ndiye anayeeneza ugonjwa wa Bancroftian Filariasis.

Anasema ilimpasa kujifunza kutambua hatua za awali za mzunguko wa maisha ya parasaiti huyo na mwingine aitwaye Onchocerca Volvulus huku akijifunza kupasua mbu kwa ajili ya ucuhunguzi wa lava wa maambukizi na utambuzi wa mabara wa parasaiti mbalimbali, kama vile wa kichocho (schistosomes), minyoo ya tumboni (hookworks), trikurisi (Trichuris).

Wakati huo, dunia yake ilikuwa dunia ya minyoo, na watu waliomuingiza katika dunia hiyo walikuwa miongoni mwa wajuzi wa mabara na wasaidizi wa mabara, ambao walimpatia mafunzo bora kabisa.

Mwele haachi kushukuru mafunzo hayo kwa sababu yamemsaidia sana kumfanya kuwa mtu aliye sasa.

Watanzania wengi wamemfahamu Dokta Mwele katitka kazi yake kubwa ya kutokomeza magonjwa yasiopewa kipuambele hususan matende na mabusha. Katika sehemu nyingi za Tanzania kama Pangani na Mtwara alijulikana kama mama matende.

Kazi hii ilimpatia nishani ya kutambulika kwa kazi hii muhimu kutoka seriakli ya marekani (Neglected Tropical Disease Champion Award). Hivi sasa takwimu za Mtwara zinaonyesha kushuka kwa ugonjwa wa matende na mabusha kutoka asilimia 60-80 mwaka 2002 hadi asilimia 0 mwaka 2014. Juhudi hizi zimeendeshwa na Watanzania wakiongozwa na Mtanzania.

PANDA SHUKA ZA TAFITI ZA MWELE

Kila jambo lina changamoto zake, katika makala mblai mbalia alizoweza kufanya, haachi kuzungumzia kuhusu changamoto kazi yake.

Mwaka 2016, kipindi cha utawala wa Hayati Magufuli, Dkt. Mwele alitoa ripoti juu ya kuwepo kwaugonjwa wa ZIKA, mapokeo hayakuwa sawa na alivyotegemea kwani Rais huyo alitengua nafasi yake ya Ukurugenzi Mkuu katika Kituo hicho cha NIMR.

Japo taarifa ya Ikulu kuhusu uamuzi huo wa Rais haikutoa sababu yoyote, ni siri ya wazi kuwa ulitokana na taarifa aliyoitoa Dkt Mwele kwa waandishi wa habari kuhusu utafiti wa virusi vya ugonjwa wa Zika.

Kwamba taarifa yake ilitafsiriwa vibaya au kulikuwa na mpango wa makusudi kumwondoa katika nafasi hiyo, ni jambo ambalo hadi sasa tunaishia kuhisi tu. Kilicho bayana ni kwamba hakutangaza MLIPUKO wa ugonjwa wa Zika bali aliripoti tu kuhusu MATOKEO ya utafiti uliofanywa na taasisi ambao ulibani kuwa sampuli 88 za damu kati ya 533 zilikuwa na virusi vya ungonjwa huo.

TanzaniaWeb