Uko hapa: NyumbaniNchiPeopleSiasaMwigulu Nchemba

Watu Maarufu Tanzania

Siasa

Mwigulu Nchemba

Waziri wa Fedha, Uchumi na Mipango

NCHEMBA PRO
Tarehe ya Kuzaliwa:
1975-01-07
Mahali pa Kuzaliwa:
Tanzania

Mwigulu Lameck Nchemba ndilo jina halisi la kiongozi huyu, Amezaliwa mnamo mwaka 1975, tarehe 7 mwezi januari katika wilaya ya Iramba iliyopo mkoa wa Singida.

Ni kiongozi wa wananchi wa Iramba Magharibi anayewaakilisha katika Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, pia ni Waziri wa Fedha, Uchumi na Mipango na ni mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM.

ELIMU

Amesoma katika shule ya Msingi ya Makunda iliyopo wilayani Iramba, na baadae kujiunga na shule ya Iboro kwa ajili ya masomo ya sekondary na kumaliza elimu ya sekondari katika shule ya Mazengo aliposoma kidato cha tano na sita.

Mwaka 2001 alianza Elimu ya juu katika chuo ikuu cha Dar es Salaam alipochukua Shahada ya Uchumi, na kuhitimu mwaka 2014 , aliunganisha masomo yake kwa kusoma Shahada ya Uzamili kwa masomo hayo hayo ya Uchumi , na baadae alijiendeleza kwa kufanya Shahada ya Uzamivu (PHD) kwa masomo hayo hayo na katika chuo hiko hiko.

SIASA NA KAZI

Kabla ya kujiunga na Siasa, Mwigulu aalikuwa akifanya kazi Benki Kuu ya Tanzania kama moja Wachumi katika benki hiyo.

Alichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Iramba tangu mwka 2010, na kuwahudumia wanachi hao tangu kipindi hicho hadi sasa.

Aliteuliwa na Rais Kikwete, kuwa Naibu wazirri wa Fedha, Uchumi na Mipango, Uteuzi huo ulichafuliwa na skendo ya Tegeta Escrow.

Baadae aliteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, hadi pale awamu ya uonggozi wa Rais Kikwete ulipokoma.

Katika uchaguzi wa mwaka 2015, alipata nafasi nyingine tena ya kuwawakilisha wananchi wa Iramba, chini ya uongozi mpya wa Hayati John Pombe Magufuli.

Aliteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria akichukua nafasi ya Dr. Agustine Phillip Mahiga, aliyefariki dunia.

Mwaka 2016 aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani nafasi aliyoishika kwa miaka miwili tu, na ilipofika 2018, Hayati Magufuli alitengua uteuzi wake na kujaza nafasi hiyo kwa kumteua Kangi Lugola.

Mwaka 2021, mara baada ya kifo cha Rais Magufuli, chini ya uongozi wa rais Samia Suluhu aliteuliwa kuwa Waziri wa Fedha, Uchumi na Mipango,akichukua nafasi ya Dkt.Philips Mipango aliyeteuliwa kuwa Makamu wa Rais.

Kwa sasa, Waziri huyu anasikika sana kufuatia kupitishwa kwa sheria mpya ya Tozo za miamala ya simu, kodi mpya ya Majengo kupitia malipo ya umeme kwa njia ya LUKU.

Mapokeo ya kodi hizi yameongeza kusikika kwa jina la Waziri huyu huku wengi wakionekana kuchukizwa na jinsi hiyo ya ukusanyaji mapato.

Hizi zaweka kuwa tu ni changamoto za kiutendaji, kwani hakuna kizuri kisicho na kasoro.

Utamtambua Mwigulu kwa uvaaji wake wa Tai yenye Rangi za Bendera ya Taifa, wakati mwingine hupendelea kuvaa wa Skafu yenye rangi hizo.

TanzaniaWeb