Uko hapa: NyumbaniNchiPeopleSiasaPalamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi

Watu Maarufu Tanzania

Siasa

Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi

Waziri wa Katiba na Sheria

5137 Prof Kabudi Pic
Tarehe ya Kuzaliwa:
1956-02-24
Mahali pa Kuzaliwa:
Singida

Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (alizaliwa 24 Februari 1956) ni mwanasheria wa Tanzania, waziri wa mambo ya sheria na katiba.

Profesa Kabudi alizaliwa katika mkoa wa Singida, alisoma katika shule ya msingi Kilimatinde kuanzia mwaka 1964 hadi mwaka 1965 na mwaka 1966 alihamia katika shule ya Kitete Primary school, na mwaka 1967 alihamia katika shule ya Berega Primary School.

Mwaka 1971 alijiunga na shule ya upili ya Tosamaganga alipomaliza kidato cha 6 mnamo 1974. Kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alisoma sheria hadi kuhitimu na shahada ya uzamili mnamo 1986. 1989 hadi 1995 alisoma Berlin, Ujerumani akapokea shahada ya uzamili (PhD) ya sheria

Alikuwa profesa ya sheria kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hadi mwaka 2017 alipoteuliwa na Rais Magufuli kuwa mbunge wa kuteuliwa na kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Mwaka 2019 alibadilishwa kazi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje hadi Mwaka 2021 aliporudishwa tena wizara ya sheria na katiba katika baraza jipya chini ya Rais Samia Suluhu.

Taarifa za Serikali