Uko hapa: NyumbaniNchiPeopleGovernment OfficialsPatrick Mfugale

Watu Maarufu Tanzania

Government Officials

Patrick Mfugale

Mkurugenzi wa TANROADS

ARON MFUGALE
Tarehe ya Kuzaliwa:
1953-12-01
Mahali pa Kuzaliwa:
Ifunda, Iringa
Date of Death:
2021-06-29
DECEASED

Mhandisi Patrick Aron Lipilima Mfugale, Alizaliwa 1/12/1953 katika eneo la Ifunda, Mkoa wa Iringa. Mhandisi na mtaalamu wa Madaraja aliejizolea sifa nyingi kwa kushiriki katika usanifu wa madaraja zaidi ya Elfu moja (1000) nchini Tanzania,yakiwemo madaraja makubwa na madogo. Elimu Mfugale Alisoma elimu ya Msingi katika shule ya Consalata Fathers Primary School iliyopo Iringa mjini . 1975 Alimaliza elimu yake ya Sekondari katika shule ya Sekondari ya Old Moshi na mnamo mwaka 1976 alijiunga na Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). Alipata Shahada ya kwanza ya Uhandisi mwaka 1983 kutoka Chuo Kikuu cha Rokii (Nchini India) iliyofuatwa na shahada ya Uzamili ya Uhandisikutoka Chuo Kikuu cha Loughbrough (Nchini Uingereza) mwaka 1995. Utumishi wake Serikalini Alianza kazi ya kuitumikia Serikali mwaka 1977, aliajiriwa Wizara ya ujenzi kama fundi sanifu msaidizi,na amehudumu katika nafasi mbali mbali ndani ya Wizara ya ujenzi. Mwaka 1983 Mfugale alichaguliwa kuwa Mhandisi mkazi wa matengenezo ya bara bara za Changarawe katika Mikoa ya Lindi,Ruvuma na Mtwara. Mwaka 1984 alichaguliwa kuwa mhandisi Mkazi wa Matengenezo ya bara bara kuu Mkoa wa Arusha. Mwaka 1986 Mfugale alipandishwa Cheo na kuwa Mhandisi Mfawidhi wa mipango na ufatiliaji wa matenegenezo ya barabara kuu nchini. Mwaka 1989 aliteuliwa kuwa mratibu wa mradi wa kitaifa wa miradi ya ujenzi wa bara bara inayofadhiliwa na wadau wa maendeleo katika mikoa ya Iringa,mbeya ,Ruvuma,Rukwa,Lindi na Mtwara. Kutokana na utumishi wake uliotukuka,Juhudi na nidhamu mwaka 1992,alipandishwa cheo kuwa Mhandisi mwandamizi wa madaraja nchini. Aliteuliwa kuwa Muhandisi mkuu wa Madaraja nchini Tanzania wakati huo, na akiwa masomoni nchini Uingereza mwaka 1995 alitafiti na kutengeneza mfumo wa madaraja hapa nchini. Alitengeneza mfumo wa usimamizi wa madaraja kwa jina la “Tanzania Bridge Management System”. Alisajiliwa kama Mhandisi mtaalamu (yaani Proffessional Engineer) mwaka 1991 na namba yake ya usajili ilikua ni 689. Mhandisi mshauri alisajiliwa mwaka 2014, na namba yake ni 325 na ni mwanachama wa Chama cha Wahandisi Tanzania. Amekua mjumbe wa bodi mbali mbali katika utumishi wake zikiwemo NCC, Road Fund Board ,MEKO na nyingine nyiingi. Injinia Mfugale ametumia muda wake mwingi sana wa utumishi kama mtaalamu wa madaraja nchini. Mfugale huyu huyu ndie Aliebuni daraja la Malagarasi lenye mita 178 kwa muda wa miezi 3 kwa shilingi za Tanzania milioni 300 wakati huo,Na kupunguza umbali wa kutoka Tabora hadi kugoma,kutoka kilomita 760 hadi kilomita 420. Injinia mfugale ameshiriki akiwa kiongozi wa wataalamu katika kusanifu na kujenga madaraja makubwa mbali mbali kwa uchache Daraja la Mkapa kwenye mto Rufiji,Daraja la Umoja linalounganisha Tanzania na Msumbiji, daraja la Rusumo mkoani Kagera, daraja la Kikwete, kwenye mto Malagarasi, daraja la Nyerere Kigamboni,Daraja la Kijazi lililopo ubungo Mkoani Dar es Salaam na madaraja mengine makubwa yaliyopo katika hatua mbali mbali. Injinia Patrick mfugale Akiwa mhandisi mkuu katika iliyokua Wizara ya Ujenzi ameongoza katika kubuni na kusimamia ujenzi wa madaraja makubwa na madogo yapatayo 1400 hapa nchini. Amebuni na kusimamia bara bara za Kitaifa mbali mbali nchini za kiwango cha lami,na licha ya kuwa alikua ni mtaalamu wa madaraj nchini vile vile mwaka 2016 aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa tume ya wataalamu ujenzi wa Reli ya kisasa Standard Gauge Railway (SGR) . Pia mwaka 2018 Injinia mfugale aliteuliwa kuongoza timu ya wataalamu wanaobuni na kusimamia Ujenzi wa Uwana wa michezo Dodoma Sports Complex katika hatua za usanifu wake,na alihusika kama mjumbe wa timu ya majadiliano ya miradi mikubwa ya umeme kama Stiglers Gauge Project,bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere. Tuzo Kutokana na mafanikio yake katika Taaluma ya Uhandisi, Mwaka 2003 alipokea tuzo kutoka kwa bodi ya usajili ya Wahandisi “Distinguished Engeneering Accomplishment Award”,na mwaka 2018 alipendekezwa kutunukiwa tuzo ya “Engineering Excellency Award”,na bodi hiyo hiyo ya usajili wa wahandisi Tanzania. Fly Over ya kwanza kutengenezwa nchini Tanzania, ilipewa jina lake kama heshima na aliekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Hayati DR. John Pombe Magufuli,na mara kadhaa alisikika akimsifu hadharani kwa uhodari na uchapakazi wake. Mpaka umauti unamfika June 29, 2021,Mfugale alikua ni Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Barabara nchini Tanzania TANROADS.Na ameitumikia serikali kwa zaidi ya miaka arobaini. Mhandisi Mfugale ameaga dunia June 29,2021 Mkoani Dodoma alipougu ghafla baada ya kuhudhuria kikao kazi na kujisikia homa akiwa ndani ya kikao,na alizikwa Julai 5,2021 Ifunda Mkoani Iringa.

Mitandao