Uko hapa: NyumbaniNchiPeopleBurudaniRuge Mutahaba

Watu Maarufu Tanzania

Burudani

Ruge Mutahaba

Mfahamu Ruge Mutahaba

MUTAHABA
Tarehe ya Kuzaliwa:
N/A
Mahali pa Kuzaliwa:
Brooklyn, New York
Date of Death:
2019-02-26
DECEASED

Ruge Mutahaba (Alizaliwa Brooklyn, New York, Marekani, 1 Mei 1970 - Alifariki Afrika Kusini, 26 Februari 2019) alikuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Vipindi wa Clouds Media Group nchini Tanzania.

Elimu Ruge ni Mtoto wa kwanza wa profesa Gelase Mutahaba na Christina Mutahaba, Ruge alipata elimu yake ya shule ya msingi mkoani Arusha darasa la kwanza hadi la sita, kisha akahamia Shule ya Msingi Mlimani ambako alihitimu elimu yake ya msingi. Baadaye alijiunga na Shule ya Sekondari Forodhani mkoani Dar es salaam na kuhitimu kidato cha nne, na kidato cha sita katika shule ya sekondari Pugu. Alihitimu shahada ya Masoko kisha Shahada ya Sanaa katika Uchumi Chuo Kikuu cha San Jose huko Kalifornia, Marekani

Taaluma Aliporejea Tanzania kutoka Chuo Kikuu cha San Jose cha California (Marekani) ambako alihitimu masomo yake, Ruge alianza kutambulika kwenye jamii baada ya kuanza kufanya kazi na rafiki yake Joseph Kusaga ambaye alikuwa akiendesha Klabu yake ya usiku almaarufu kama disko iliyokuwa ikijulikana kwa jina la Clouds Disco.

Ushirikiano wao ulipelekea kuanzishwa kwa Clouds Media Group mjini Arusha ambayo, licha ya kuwa chombo cha habari na burudani kwa jamii, hasa vijana, ilifanya kazi ya kuhamasisha vijana wadogo wa Kitanzania kujiingiza katika kutafuta fursa na ujasiriamali ili kujiinua na kuchangia katika maendeleo ya jamii zao na taifa kwa ujumla wake.

Tokea maisha ya utotoni Ruge alikuwa mpenada muziki, lakini kipaji chake hakikuwa kwenye muziki peke yake. Alikuwa mchezaji mpira wa miguu (soka), alipewa majina mengi kwa kipaji hicho akicheza timu za mtaani, za Chuo Kikuu kuanzia Adanco na Summer Rangers na alifikia hatua ya kuchaguliwa katika timu ya mkoa wa Dar es salaam ya UMISETA. Pia alikuwa na kipaji cha kuandika. Vipaji vingine vyote havikuweza kunawiri kwani alikuwa na mapenzi na muziki zaidi.

Familia Ruge Mutahaba hakuwahi kufunga ndoa rasmi lakini alikuwa na mahusiano na Zamaradi Mketema na walipata watoto wawili. Pia alizaa wengine watatu na kufanya jumla ya watoto watano(5)[5

Maradhi na kifo Ruge Mutahaba alikuwa akisumbuliwa kwa muda mrefu na tatizo la figo, Ruge alipelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu, ambayo pia alyekuwa rais wa Jamhuri ya Tanzania Hayati John Magufuli alimchangia shilingi milioni hamsini , hadi mauti yalipomfika tarehe 26 Februari 2019.

Watanzania wengi waliopokea habari za kifo chake, akiwemo Hayati John Pombe Joseph Magufuli, walishtushwa na habari za mauti yake na kutuma jumbe za kuguswa kutokana na mchango mkubwa wa Ruge katika tasnia ya habari na burudani, ubunifu katika mipango mikakati, kuendeleza vipaji vya vijana wa Tanzania, kuhamasisha ari ya ufanyaji kazi kwa bidii katika jamii na maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Wafanya kazi wa Clouds walimlilia sana huku wakimpa jina Jasiri Muongoza Njia kwakua uwezo wake ulikuwa wakipeke kazini. wasanii wengi wa bongo fleva waliuzunishwa na msiba huo. Ruge alikuwa mtu wa watu kila mtu aliezea mchaango wa Ruge kwenye maisha yake. Ni dhahiri kua aligusa maisha ya watu wengi sana .

TanzaniaWeb