Uko hapa: NyumbaniNchiPeopleTraditional RulersSimon Sirro

Watu Maarufu Tanzania

Traditional Rulers

Simon Sirro

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP

Frnt Sirro1
Tarehe ya Kuzaliwa:
1963-00-00
Mahali pa Kuzaliwa:
Tanzania

Simon Nyakoro Sirro, ni mtumishi wa jeshi la polisi nchini Tanzania, akihudumu kwa sasa kama Inspekta Jenerali Mkuu wa jeshi hilo.

Amezaliwa eneo la Kiabakari, lililopo wilaya ya Butiama mkoani Mara mwaka 1963.

Kuhusu Elimu yake, Simon Sirro, amesoma shule ya sekondari ya Iliboru iliyopo jijini Arusha, na Tosamaganga kbla na kuchukua Shahada ya awali ya Sheria.

alisoma pia Seminari akiwa anchukua masomo ya Upadri, na kufika ngazi ya juu kabla ya kuacha na kujiunga na Jeshi la Polisi.

UTUMISHI NDANI YA JESHI LA POLISI

Sirro amewahi kuwa Mkuu wa Upelelezi Kituo cha Polisi Buguruni mwaka 1998, Mkuu wa Upelelezi Tarafa ya Magomeni kwa miaka 5 na Mkuu wa Upelelezi Msaidizi Mkoa wa Tabora.

Mwaka 2002 alikuwa Mkuu wa Upelelezi Msaidizi Mkoa wa Dar es Salaam akiwa ni msaidizi wa Abdallah Zombe.

Sirro ni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam wa tatu ambapo aliteuliwa na Rais Dkt Magufuli Februari 15 mwaka 2006 akichukua nafasi ya Suleiman Kova aliyeshika wadhifa huo tangu mwaka 2008. Kabla ya Kova aliyekuwa akiongoza Kanda Maalum ya Dar es Salaam ni Alfred Tibaigana.

Wakati Suleiman Kova akiongoza Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Sirro alikuwa msadizi wake ambapo baadae alirithi mikoba yake.

Kabla ya kuongoza Kanda Maalum Dar es Salaam, Sirro amewahi kuwa Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Tanzania. Moja ya opersheni kubwa alizowahi kuongozi ni Operesheni Kimbunga dhidi ya wahamiaji haramu mwaka 2012.

Lakini pia, Simon Nyakoro Sirro amewahi kuwa Kamanda wa Polisi wa Mikoa mbalimbali ambayo ni Tanga, Mwanza na Shinyanga.

Anakuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wa 10 wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, mara baada ya kuteuliwa Mkuu wa Jeshi la Polisi mwaka 2017 chini ya uongozi wa Hayati Magufuliakichukua nafasi ya Ernest Mangu.

Mapema tu mara baada ya uteuzi huo, Kamanda Sirro, alifanya mabadiliko katika safu ya uongozi wa Jeshi la Polisi kwa kuteua Makamanda wa mikoa wapya .

TanzaniaWeb