Uko hapa: NyumbaniNchiPeopleMichezoSunday Manara

Watu Maarufu Tanzania

Michezo

Sunday Manara

Mcheza Soka Mstaafu

Sun Man
Tarehe ya Kuzaliwa:
1952-11-23
Mahali pa Kuzaliwa:
Kigoma

Anatoka katika Familia ya wanasoka, na mchezaji wa kwanza kucheza ligi moja na Edson Arantes do Nascimento maarufu kama Pele, Gwiji wa Soka Ulimwenguni, huyu ni Sunday Manara, Gwiji na alama ya Soka la Tanzania.

Kuzaliwa

Anaitwa Sunday Ramadhan Manara alizaliwa mkoani Kigoma, Novemba 23, 1952 Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Klabu za Tanzania, Yanga na Pan African.

Elimu

alipata Elimu yake ya Msingi na Shule ya Upili huko huko Mkoani Kigoma.

Safari yake ya Soka

Young Africans ndio ambayo imempa umaarufu zaidi katika miaka ya 1968 mpaka 1972 akianzia timu ya watoto ya Yanga kids, mwaka 1969 akapandishwa timu ya Vijana ya Yanga B na kupanda mpaka kikosi cha kwanza na baadae ndio akaenda kucheza Soka katika la Kulipwa katika nchi mbali mbali barani Afrika na Ulaya.

Kuhusu Jina la "Computer"

Sunday Manara anaseam hakumbuki hasa aliempatia jina hilo ila tu anachokumbuka ni kuwa alipewa jina hilo kutokana na uwezo wake wa kufanya maamuzi ya haraka sana uwanjani pindi anapokuwa na mpira.

Aliwezaje kwenda kucheza soka ulaya wakati haikuwa jambo rahisi kwa kipindi kile ?

Mwaka 1976 kuna Timu inayoitwa FC Molde kutoka nchini Norway chini ya Mwalimu wake Jeck Johson ilikuwa wageni wa Simba na ilikuja nchini kwa minajili ya kucheza na Simba na katika mechi yao walitoa suluhu.

Wakati walipokuja kucheza na Yanga wachezaji wengi walikua timu ya taifa wakati huo, Sunday hakuitwa timu ya Taifa. Hivyo Timu B, ya Yanga ikapelekwa kucheza na FC Molde na sunday akijumuishwa na Yanga kushinda magoli 3-1 huku Sunday akifunga goli 2.

Kiwango alichokionyesha Sunday Manara ndicho kilichomfanya Jeck Johnson kuulizia habari za Sunday kwa wenyeji ndizo zilizomchanganya kocha huyo kwani sifa zilikua nyingi kupita kiasi.

hivyo wakamfata na kumwambia wanampeleka Denmark kwa majaribio kisha watampeleka Ulaya na huo ndio ukawa mwanzo wa Safari yake kwenda barani Ulaya.

Akiwa nchini Uholanzi katika klabu ya Heracles Sunday Manara alicheza msimu mzima wa Ligi kuu Uholanzi.

Alipotoka Uholanzi akaenda Marekani katika klabu ya New York Eagles ambapo huku alikwenda kucheza Ligi moja na Gwiji wa Soka ulimwenguni Pele ambae alikuwa akiichezea Cosmos, lakini zote zilipatikana katika Jimbo la Manhattan, New York.

Katika safari yake ya Soka Sunday Manara amevichezea vilabu tofauti tofauti kwa mafanikio Makubwa.

Young Africans, Nyota (Morogoro), 1979 Pan African SC, 1979/80 Heracles (Uholanzi), 1980/81 New York Eagles (Marekani), 1981/82 SV St. Veit (Austria) , Al-Nasr (Falme za kaiarabu) ambapo ndipo alipostaafia mwaka 1984. Aliichezea Timu ya Taifa kuanzia mwaka 1970 mpaka 1976.

Familia

Mzee Sunday alibahatika kupata watoto saba lakini mmoja ni marehemu kwa sasa.Huku mtoto wake wa mwisho pekee ndio akionekana kwa karibu kufuata nyayo za baba yake.

Mtoto wake wa Pili ni Haji Manara, aliepata kuwa msemaji wa Simba SC kati ya mwaka 2015 mpaka Julai 2021. Ikumbukwe Yanga ni Mpinzani wa Jadi wa Simba SC.

Sunday Manara anatajwa kama ndio Mtanzania wa Kwanza mwenye mafanikio zaidi pembeni ya Mbwana Samatta.

Sunday Manara vile vile ni Shabiki mkubwa wa Young Africans, na mara kadhaa ameonekana katika matukio yanayoihusisha klabu hiyo.

Familia yao ilitoa Wanasoka wengi waliocheza mpaka Timu ya Taifa akiwemo Kassim Manara na Kitwana Manara.

Mitandao